Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Koplo Grace Ndyamukama akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Dawati la Jinsia. Kulia ni Mama wa mtoto Nasra Khalfan.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka akimpa zawadi ya dawa ya meno, maji ya kunywa na juisi Hadija Selemani ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Dawati la Jinsia.
Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Rhoda Israel akimpa zawadi ya juisi Sada Issah ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Dawati la Jinsia.
Maafisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli wakigawa zawadi za maji ya kunywa, dawa za mENO, juisi, mafuta ya kupakaa, sabuni za kuogea na kufulia kwa watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Dawati la Jinsia.
Maafisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea Taasisii ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kugawa zawadi za maji ya kunywa, dawa za meno, juisi, mafuta ya kupakaa, sabuni za kuogea na kufulia kwa watoto waliolazwa katika taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Dawati la Jinsia.
Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Jane John akimpa zawadi za maji ya kunywa, dawa ya meno, juisi, mafuta ya kupakaa na sabuni Maimuna Daud ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Dawati la Jinsia.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka akiongea jambo na wagonjwa walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Dawati la Jinsia.
Picha na JKCI
ASKARI
wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli mtandao wa Polisi wanawake Dawati la jinsia wamewatembelea
na kuwagawia zawadi mbalimbali watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete kwa ajili ya matibabu ya moyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari hospitalini hapo , Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni
Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka alisema wamewatembelea wagonjwa hao
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
“Tumekuja
kuwatembelea na kuwagawia vitu mbalimbali ikiwamo sabuni za kuogea na kufulia,
dawa za meno, maji ya kunywa, juisi na vitu vingine ambavyo vyote vina thamani
ya zaidi ya shilingi laki nne,” alisema.
ASP
Mdinka aliongeza pia kutembelea Taasisi
hiyo kumewapa nafasi ya kumtembelea na kumsalimia mtoto
Salome ambaye amelazwa hospitalini hapo kwa ajili ya kutibiwa ugonjwa wa moyo.
“Salome
tulimpokea katika kituo cha Reli tukamleta hapa JKCI kwa ajili ya matibabu lakini
familia imemtelekeza licha ya kwamba ametibiwa na anaendelea vizuri,” alisema.
Aliongeza
“Bado yupo hapa hospitalini, tunaendelea kushirikiana kwa ukaribu na vyombo
vingine ili kuhakikisha anapata sehemu ya kujisitiri ili aweze kuendelea na maisha
yake kama watoto wengine, apate haki zake za msingi ikiwamo elimu,”.







0 Comments