Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akiangalia silaha ambayo imeshahakikiwa, alipotembelea
banda la Kitengo cha Ukaguzi wa silaha wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya
Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo
cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Wapili kushoto
ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akisikiliza maelezo ya jinsi silaha
inavyohakikiwa kutoka kwa Afisa wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Udhibiti wa Silaha, Dotto
Shilogile, alipotembelea mabanda ya maonesho wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10
ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya
Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akisikiliza maelezo ya uendeshaji salama wa
vyombo vya moto kutoka kwa Koplo Faustine Nduguru, alipotembelea banda la
askari wa usalama barabarani, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mtandao wa
Polisi Wanawake Tanzania, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma
za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akizindua kitabu kinachoeleza Historia ya Miaka
10 tangu kuanzishwa Mtandao wa Polisi Wanawake wakati wa Maadhimisho ya Miaka
10 ya mtandao huo, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za
Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Waziri Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa
Polisi Wanawake Tanzania,Kamishna Alice Mapunda
Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni(kushoto), akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Miaka
10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika leo
katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es
Salaam.Anayeshuhudia kushoto ni Kaimu
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Kamishna Mussa Ali Mussa.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani(wapili kulia), akimkabidhi
cheti mmoja wa askari mstaafu alietoa mchango wake wakati wa uanzishwaji wa
Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania , wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya
mtandao huo, yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi,
Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Kulia ni Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Kamishna Mussa
Ali Mussa.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani, akiongozana na Naibu
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) na Mkuu wa
Jeshi la Polisi Mstaafu, Alhaji Omari Mahita (kulia), kuelekea kukagua mabanda
wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania,
yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma za Polisi, Barabara ya
Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi







0 Comments