Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa wajasiriamali.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa wajasiriamali.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na
wananchi wa Dodoma wakati akikabidhi mashine kwa wajasiriamali Dodoma
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa na
viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani katika hafla ya kukabidhi mashine
mbalimbali kwa vikundi vya wajasiriamali.
Mashine zilizokabidhiwa kwa vikundi vya wajasiriamali
Wananchi waliohudhuria katika makabidhiano ya mashine.
……………
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini
Anthony Mavunde leo amekabidhi mashine mbalimbali kwa wajasiriamali wa
vikundi 31 na kuwataka kuhakikisha wanazitumia kwa kujiongezea kipato na
kuenda sambamba na azma ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa
Viwanda.
Akizungumza na wanavikundi hao na
wakazi wa Dodoma, Mavunde amesema mashine hizo zimenunuliwa kupitia
fedha za mfuko wa jimbo na kwamba dhamira yake ni kuhakikisha wananchi
wanajikwamua kiuchumi kwa kubadili maisha yao.
“Leo Tumegawa mashine hizi
mkazitumie zibadilishe maisha yenu msizifungie stoo zikajaa vumbi na
msipozitumia kwa malengo yaliyokusudiwa hamuwezi kufikia malengo
yenu,Mashine hizi zikaunge mkono falsafa ya Rais ya uanzishaji wa
viwanda ili kufikia uchumi wa viwanda,”amesema Mavunde
Hata hivyo amewahakikisha kuwa
amejipanga kuhakikisha anawakwamua wananchi wake kiuchumi kupitia fursa
mbalimbali na kwamba anakuja na mradi wa kuchimba mabwawa ya kufugia
samaki.
“Kuna teknolojia imekuja ya kufuga
samaki ambayo unaweza kufuga nyumbani, hiyo ndo mipango ya ofisi ya
Mbunge ya kuwawezesha wananchi kiuchumi na pia kwa upande wa kilimo
nimetafuta wataalamu kutoka India tunaangalia eneo la Nzasa kulitumia
kwa majaribio ya kilimo cha mboga mboga na ufugaji samaki,”amesema
Mavunde amesema dhamira yake ni
kuwafanya wananchi wa Dodoma wanufaike na ujio wa serikali mkoani humo
kupitia fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.
Akizungumzia kuhusu kilimo cha
Zabibu, Mavunde amewataka kuchangamkia fursa ya kilimo cha zabibu kwa
kuwa ni fursa pekee ya kuikwamua kiuchumi Dodoma ikiwa ni pamoja na
uanzishaji wa viwanda vidogo vya kukamua mchuzi wa zabibu.
“Maana kwasasa utambulisho wa
Dodoma ni ombaomba na wavivu badala ya kutambulika kwa kilimo cha
zabibu, ndugu zangu duniani kote Dodoma ni miongoni mwa maeneo
yanayovuna zabibu kwa mwaka mara mbili ni vyema tukatilia mkazo kilimo
hichi ili kuwa utambulisho wetu,”amesema
Mbunge huyo amesema kupitia
mshahara wake anatarajia kununua mashine za kukamua mchuzi wa zabibu
kutoka nchini Canada kwa kila kata kwa kuwa mchuzi huo una soko kubwa.
Amewahamasisha wananchi kupitia
vikundi walivyo navyo kuendelea kuwasilisha maombi yao na Ofisi ya
Mbunge itaendelea kununua mashine kwa awamu.
Naye, Mwakilishi wa Umoja wa
wajasiriamali Silvesta Wambura amemshukuru Mbunge huyo kwa dhamira yake
ya kuwainua kiuchumi na kudai kuwa amekuwa mkombozi wa wanadodoma.
Amesema Mbunge huyo ni chombo sahihi na mwenye ubinadamu na wananchi wana matarajio makubwa kupitia yeye.
Kwa upande wao, madiwani wa kata
za jimbo hilo wamempongeza na kumshukuru Mavunde kwa dhamira yake ya
kuwakwamua wananchi kiuchumi.






0 Comments