Waziri wa Nishati wa Tanzani,
Dkt. Medard Kalemani (kulia) na Waziri
wa Nchi anayeshughulikia Nishati kutoka
nchini Uganda, Dkt. Simon Du' Ujanga
wakitia saini ripoti ya mkutano huo.
Wanaoshuhudia wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki upande wa Sekta za Kijamii na Uzalishaji, Christophe Bazivamo na wawakilishi wa
Mawaziri wa nchi wanachama.
Makatibu Wakuu wa nchi wanachama wakisaini ripoti iliyojadiliwa katika
mkutano huo. Kwa upande wa Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Nishati
kutoka Wizara ya Nishati James Andilile amemwakilisha Katibu Mkuu Wizara hiyo.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza jambo wakati wa
mkutano huo. Wanaomsikiliza ni ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano huo.
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo kutoka nchi
mbalimbali za Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akisalimiana na
Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi mbalimbali zinazohusika
na Masuala ya Nishati na Zanzibar baada ya kukamilika kwa mkutano.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza
kulia) akiwa na Wataalam mbalimbali
kutoka Wizara ya Nishati na Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC)
mara baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano
wa 12 wa Baraza la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbele, washiriki kutoka nchi ya Rwanda wakiwa katika
Mkutano huo.
Waziri wa Nishati wa Tanzani, Dkt. Medard Kalemani
(kulia) na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Nishati kutoka nchini Uganda Dkt. Simon Du' Ujanga wakitia saini ripoti ya
mkutano huo.
Mkutano wa 12 wa Baraza la
Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 30 Oktoba,
2017 Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Jijini
Arusha, umehitimishwa leo na Kikao cha Mawaziri wa nchi Wanachama.
Kikao cha Mawaziri kilitanguliwa na Vikao vya Wataalam wa Sekta ya Nishati ,
Kikao cha Kamati ya Nishati ya Baraza hilo na Kikao cha
Makatibu Wakuu wa nchi husika.
Katika kikao cha Mawaziri,
viongozi hao pia wametia saini ripoti iliyojadiliwa katika vikao hivyo ambapo
masuala kadhaa yakiwemo ya miradi ya Umeme ya mipakani, miradi ya umeme ya nchi
na nchi, Mafuta, Gesi , Nishati Jadidifu , Sera ya Usalama wa Nishati
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na mambo mengine yalijadiliwa.
Awali, kabla ya Mawaziri wa nchi
wanachama kutia saini ripoti hiyo, pia
ilisainiwa na Makatibu Wakuu wa nchi wanachama.
Akizungumza katika mkutano huo,
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa Sekta za Kijamii na
Uzalishaji, Christophe Bazivamo ameeleza
umuhimu wa kikao cha Mawaziri na kueleza kuwa, ndiyo kikao ambacho kinatoa
mwelekeo wa utekelezaji wa yale yanayokubaliwa na nchi wanachama. Aidha,
Bazivamo ameendelea kusisitiza kuhusu umuhimu wa nishati kwa ajili ya maendeleo
ya nchi jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkutano huo
ambaye ni Waziri wa Nchi
anayeshughulikia Nishati kutoka nchini Uganda, Dkt. Simon D' Ujanga, amesema
kuwa, Viongozi wa nchi zote za Jumuiya hiyo wanayo nia ya kuhakikisha kwamba
miradi iliyokubaliwa na jumuiya inatekelezwa,
Pia amewataka nchi wanachama
Kwa upande wake, Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewashukuru wataalam wote ambao wamefanikisha
kukamilika kwa ripoti ambayo itawezesha makubalino yaliyofikiwa kutekelezwa na
jumuiya hiyo na kuongeza kuwa, yote yaliyojadiliwa katika mkutano huo yanagusa
nchi zote na hivyo yanapaswa kuchukuliwa
kwa uzito.
Nchi
zilizoshiriki mkutano huo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.
Aidha, Mwenyekiti wa mkutano huo ilikuwa nchi ya Uganda na Katibu nchi ya
Rwanda.
Tanzania katika mkutano husika
imewakilishwa na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Wizara ya Maji, Mazingira na
Nishati ya Zanzibar, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati
Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na
Wakala wa Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta , Zanzibar (ZURA).








0 Comments