Random Posts

Waziri ummy asema wananchi wasiuziwe damu

 Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam akiwa na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem
 Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizindua Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam akiwa na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem
 Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem kulia akimkabidhi zawadi ya mchango mkubwa katika Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu kushoto wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam.
 Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem.
 Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem aliyesimama akiongea na baadhi ya  wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam , katikati waliokaa ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Lwezimula.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Mifupa nchini MOI wakimsikiliza kwa makini ni Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait leo jijini Dar es salaam.
 Mwanachama wa Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa  Wanawake (WOW) Afrika Mashariki Bi. Rehema Mwangolombe akiwa katika maandalizi ya kuchangia damu  damu katika Benki ya damu mpya iliyozinduliwa na Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi huo uliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem akichangia damu katika uzinduzi wa benki ya damu leo.

PICHA NA ALLY DAUD- WAMJW
......
NA  WAMJW-DAR ES SALAAM.
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  ameendelea kusisitiza kuwa wananchi hawapaswi kununua damu kwani huduma hiyo ni bure kwa watanzania wote katika hospitali zote.

Hayo amezungumza leo jijini Dar es salaam  wakati wa  uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait katika Taasisi ya Mifupa MOI ambapo uliuzuliwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania.

“Watanzania wanahoitaji huduma ya kuongezewa damu wapewe bure marufuku kwa watoa huduma za vituo vya afya pamoja na hospitali zote kuuza damu hiyo kwani inatoka kwa wananchi wenyewe” alisisitiza Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza katika kuchangia damu ili kuweza kuwa na hifadhi ya kutosha na kufanya kazi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kwa wakati sahihi bila ya usumbufu wowote katika kuokoa maisha ya watanzania.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema  kuwa anayo furaha kutimiza miaka miwili tangu kuingia kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kupiga hatua katika sekta ya afya hasa katika kupunguza rufaa za nje na kuwa na utaalamu wa matibabu ya kibingwa kama vile upandikizaji wa figo, vifaa vya usikivu( Coclea Impant) na kutibu magonjwa ya moyo.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem amesema kuwa  wameamua kuchangia kiasi cha fedha cha shilingi Milioni 200 katika kutengeneza Benki hiyo ya damu MOI ili kuweza kusaidia kuboresha sekta ya afya nchini.

“Mbali na kiasi hicho cha fedha pia tumetoa Dola za Kimarekani 500 ili kuweza kusaidia  walemavu mbalimbali katika kulejesha hali zao za kawaida hapa nchini” alisema Bw. Al-Najem.

Aidha katika uzinduzi huo wa Benki ya damu Balozi Al-Najem alijitolea damu unit moja ili kuweza kuchangia benki hiyo ya taasisi ya Mifupa MOI ili kuweza kuhamasisjha na wananchi wengine waweze kuchangia damu kwa msaada wa wagonjwa wengine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Lwezimula alisema kuwa katika kuhakikisha Matibabu ya kibingwa yanapiga hatua nchini waliamu kuanzisha kambi za matibabu kuanzia mwaka 2000 na kufanya taasisi zingine za afya kuiga mfano huo.

“Tunataka kuhamasisha matibabu ya kibingwa kufanyika nchini pamoja na uchangiaji damu kwani damu hiyo haitatumika MOI peke yake bali hata kwenye Taasisi zingne na vituo vya Afya nchini kote” alisema Dkt. Lwezimula.

Sambamba na tukio hilo Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa  Wanawake (WOW) Afrika Mashariki walijitolea kuchangia damu ili kuweza kusapoti benki hiyo kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ya damu.


“Tumehamasika kuja kuchangia damu ili kuweza kutoa mfano kwa wanachi wengie waweze kujitolea katika uchangiaji huu wa damu ili kujenga taifa lenye watu wenye afya bora” alisema Mkurugenzi wa WOW Bw. Martin Gabone.

Post a Comment

0 Comments