Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akimsikiliza Meneja wa TANESCO Mkoa wa TEMEKE,
Mhandisi Jahulula Jahulula katika moja ya maeneo kunakotekelezwa Miradi ya
TANESCO, Mbagala. Wengine ni Wataalam kutoka TANESCO na Wizara ya Nishati.
Meneja
wa TANESCO Mkoa wa TEMEKE, Mhandisi Jahulula Jahulula (kushoto) akimwonesha
Naibu Waziri line za umeme katika moja ya maeneo ambayo TANESCO inatekeleza
miradi yake, eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam. Wengine ni Wataalam kutoka
TANESCO na Wizara ya Nishati.
Meneja
wa TANESCO Mkoa wa TEMEKE, Mhandisi Jahulula Jahulula (aliyenyoosha mkono)
akimweleza jambo Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu. Wengine ni Wataalam
kutoka TANESCO na Wizara ya Nishati.
Meneja
wa TANESCO Mkoa wa TEMEKE, Mhandisi Jahulula Jahulula (aliyenyoosha mkono)
akimwonesha Naibu Waziri moja ya Transfoma zilizofungwa katika eneo la Mbagala.
Wengine wanaofuatilia ni Wataalam kutoka TANESCO na Wizara ya Nishati.
Na
Asteria Muhozya, DSM
Naibu
Waziri wa Nishati Subira Mgalu ametembelea Miradi ya Umeme inayotekelezwa na
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika maeneo tofauti eneo la Mbagala
jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi
hiyo.
Naibu
Waziri ameyasema hayo leo tarehe 5 Oktoba, 2017, alipotembelea miradi
mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo eneo la Mbagala, ikiwemo uwekaji wa
line mpya, na ufungaji wa Transfoma.
Aidha, ameitaka TANESCO kubuni njia
zitakazowezesha kuwaunganisha wananchi na nishati ya umeme kutokana na mahitaji
ya nishati hiyo kuwa kubwa katika eneo la Mbagala na maeneo mbalimbali nchini.
“Kadri
miradi inavyotekelezwa ni vema wakafanya
makisio kuendana na uongezeko la wateja lakini wazingatie ubunifu. Mfano zipo nyumba ambazo zimejengwa
baada ya mradi kutekelezwa. Ni vema TANESCO ikajipanga kuona namna ya
kuwahudumia wateja wapya,”amesisitiza Naibu Waziri.
Pia,
Naibu Waziri amewataka wananchi ambao bado hawajafikiwa na huduma hiyo, kuanza
kujipanga ili pindi miundombinu ya umeme inapofika katika maeneo yao waweze
kuunganishwa na nishati hiyo.
Aidha,
Mgalu ameeleza kuridhishwa na namna shirika hilo linavyotumia mapato yake
kutelekeza miradi mbalimbali, lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba, wananchi
wanaunganishwa na nishati hiyo.
Miradi
hiyo ya ujenzi wa njia za umeme za msongo wa kilovolti 11 kila eneo,
inatekelezwa katika maeneo tofauti ya Chamazi Dovya 1- 3, Mbande kwa Masista
1-3, kwa Mzala na Chamazi Vigoa.
0 Comments