Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage akizungumza na
viongozi wa vyama vya siasa kwenye mkutano wa Tume na vyama hivyo ikiwa ni
maandalizi ya uchaguzimdogo wa Novemba 26, 2017.Mkutano huo umeliofanyika leo jijini Dar
es Salaam leo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mst. Hamid Mahmoud Hamid na kulia
ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi Kailima Ramadhani akitoamada kwa viongozi wa vyama vya siasa wakati
Tume ilipokutana na vyama vya siasajijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (wa tatukulia)
akiwamezakuu na Makamu Mwenyeki tiJaji Mst. Hamid Mahmoud Hamid( wa tatukushoto),
Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani )wa pilikulia), Makamishna wa NEC
JajiMst. Marry Longway na AsinaOmari na kulia ni Mwakilishi wa Mkuuu wa Jeshi
la Polisi (IGP),kwenye mkutano wa Tume na vyama vya siasauliofanyikaDar es
Salaam jijinileo.
Baadhi
ya viongozi wavyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage kwenye mkutano wa Tume na vyama vya
siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Yeremia Maganja akichangia mada kwenye mkutano
wa Tume na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi Kailima Ramadhani akizungumza na waandishi wa Habari baada ya
ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na vyama vya
siasauliofanyikajijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekitiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles
Kaijage (kushoto) akisalimiana na
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Pwani
Casimirmabina.Katikati ni Kaimu KatibuMkuu wa Chama cha UDP Saumu Rashid.
Pichana
Hussein Makame-NEC
Hussein Makame-NEC
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistolces
Kaijage amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili ya
Uchaguzi.
Jaji Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa NEC na
vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kuelekea Uchaguzi mdogo wa
madiniwa.
Alisema iwapo ukiukwaji au uvunjaji wa Maadili hayo
utatokea, Chama au Mgombea awasilishe malalamiko hayo mbele ya Kamati husika
ili ishughulikiwe kisheria.
Aliwakumbusha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 53 cha Sheria ya
Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Tume inayo mamlaka ya kuruhusu
kuwepo kwa Kampeni za Uchaguzi katika maeneo ya Uchaguzi na siyo Mikutano ya
Vyama vya Siasa.
Hivyo, kampeni hizo zifanyike kwenye Kata husika na inategemewa
kuwa Mikutano ya Kampeni italenga kuwashawishi, kwa namna ya kistaarabu,
wananchi wa Kata husika ili wamchague Mgombea anayefanyiwa kampeni.
” Kwa mujibu wa kipengele cha 2.1. (c) cha Maadili ya Uchaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 tunategemea kila Chama cha Siasa
kiendelee kufanya Kampeni kwa mujibu wa ratiba. Kampeni zote zinatakiwa kuanza
saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni” alisema Jaji Kaijage.
Aliongez kuwa kwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge
na Madiwani ya mwaka 2015, Tume imekwisha kutoa ushauri kwa Viongozi wa Mikoa
na Wilaya ili katika kipindi hiki cha Uchaguzi wahakikishe wanazingatia wajibu
wao na ukomo wa madaraka yao katika shughuli za Uchaguzi kuanzia kipindi cha
Kampeni hadi kutangazwa kwa Matokeo.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi kailima Ramadhani aliaviomba Vyama vya
Siasa kuwahimiza wanachama na wapenzi wao walioandikishwa kuwa Wapiga Kura
wajitokeze Siku ya Uchaguzi kwenda Kupiga Kura zao bila hofu yoyote
kuhusu usalama wao.
“Ni imani ya Tume kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa mtakuwa chachu
ya kuwaongoza na kuwaelekeza wanachama, wafuasi na mashabiki wenu katika
kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu’ alisema Kailima.
Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika kata 43 za Tanzania Bara,
unatarajiwa kufanyika tarehe 26 Novemba, 2017 ambapo wapiga kura 333,309
wanategemewa kupiga kura siku ya uchaguzi huo.







0 Comments