Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bibi. Joyce Hagu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bw. Benson Mkenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Jason’s TV Bw. Sanctus Mtsimbe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) wakifuatilia yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi JTV Bw. Sanctus Mtsimbe
Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akibonyeza rimoti kuzindua Chaneli ya Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiangalia Chaneli ya Jason’s TV (JTV) baada ya kuizindua jana Jijini Dar es Salaam. JTV itakua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inapatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126.
Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(waliokaa katikati) katika
picha ya pamoja na wadau wa sekta ya filamu baada ya kuzindua Chaneli
ya Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na
inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana
Jijini Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
…………..
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Wadau mbalimbali ndani na nje ya
nchi wametakiwa kujitokeza na kuwekeza katika vifaa vya kisaa vya
kurekodia filamu ili sekta ya filamu nchini Tanzania iweze kuendelea
zaidi na kuvuka mipaka kwa kuwa na ubora wa kuweza kushindana na filamu
za nchi nyingine.
Rai hiyo imetolewa na Rais Mstaafu
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
alipokua akizindua chaneli mpya ya Jason’s Televisheni itakayokuwa
ikionyesha filamu mpya za kitanzania inayopatikanakatika king’amuzi cha
Star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
“Wadau wa tasnia ya filamu nchini
hasa waandaaji wa filamu mnapaswa kuangalia namna ya kupata wadau
watakaosaidia kuwekeza vifaa vya kisasa vya kurekodia na kwa upande
wangu nitajaribu kuwakutanisha na wadau wenye uwezo wa kuwekeza ili
muangalie namna ya kuzungumza nao na kuwekeza vifaa vitakavyowawezesha
kuandaa filamu zenye ubora na kukidhi hadhi ya kushindana kimataifa”
amesema Mhe. Kikwete.
Aidha Mhe. Kikwete amesema kuwa
kuwepo kwa chaneli ya JTV itakayokua ikirusha filamu mpya za kitanzania
ni jambo muhimu sana katika historia ya tasnia ya filamu hapa nchini
hivyo uzinduzi wa chaneli ya JTV unafungua ukurasa mpya katika maendeleo
ya tasnia ya filamu ambayo imekua ikikua kwa kasi.
Mhe. Kikwete amesema kuwa
kufanikiwa kwa chaneli ya JTV kutapunguza machungu mengi ya
watayarishaji wa filamu kwa kutatua changamoto ya kutokuwa na soko la
uhakika na kuleta nuru ya matumaini kwa wasanii kwa kupata malipo
yanayostahili kwa vipaji vyao, jasho lao pamoja na gharama wanayoingia
katika kutengeneza filamu.
Kwa upande wake Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa
uanzishwaji wa chaneli ya JTV ni moja ya mikakati kadhaa ya kuboresha
usambazaji wenye tija wa filamu mpya za kitanzania hivyo kuwataka
watayarishaji wa filamu kuthamini mandhari za filamu zetu kwani filamu
iliyokosa hata dakika moja kuonyesha vivutio vya utalii tulivyonavyo
inakosa sifa ya ubora.
Awali Mhe. Mwakyembe amesema kuwa
Tanzania itabaki kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya
10 kuzungumzwa na watu wengi duniani kati ya lugha 6000 hivyo ni
matarajio ya wizara baada ya muda mfupi mtu akisikia ala za nyimbo za
Kiswahili katika filamu zetu kama vile Mdumange, Sindimba nk. ajue
anaangalia filamu ya kitanzania.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Bw. Benson Mkenda amesema kuwa bodi ya filamu ipo tayari
kushirikiana na wadau wote katika tasnia ya filamu wenye nia ya kukuza
na kuendeleza tasnia kama ilivyo kwa Jason’s TV ambao lengo lao mahususi
limelenga kuendeleza sekta ya filamu hasa katika eneo la usambazaji ili
kuweza kuitoa sekta hii mahali ilipo na kuifikisha katika viwango vya
kimataifa.









0 Comments