Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa
Fedha- IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es
Salaam, Dkt. Philip Isdor Mpango Mb), akihutubia Jumuiya ya wanachuo
hicho ambapo aliwatunuku vyeti wanafunzi 2692 waliohitimu kozi
mbalimbali katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya
jamii.
Mwenyekii wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Prof.
Lettice Rutashobya, akihutubia wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha
Usimamizi wa Fedha- IFM yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee,
Jijini Dar es Salaam, ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali
katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Prof. Tadeo Satta,
akihutubia wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM,
yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam,
ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha,
uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
Meza Kuu wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) wakiimba Wimbo wa Taifa
wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM,
yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam
ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika Nyanja za Fedha,
Uhasibu, Bima, TEHAMA na Hifadhi ya Jamii. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo hicho Prof. Lettice Rutashobya na wa Pili kulia ni Mkuu
wa Chuo hicho Prof. Tadeo Satta.
Baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa
Fedha- IFM, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar
es Salaam, wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati
wa mahafali hayo ambayo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, waliofanya vizuri
zaidi katika masomo yao wakipokea zawadi ya hundi kifani yenye thamani
ya shilingi 1,200,000 ambayo ni sehemu ya zawadi lukuki walizopewa
wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo hicho, yaliyofanyika katika ukumbi wa
Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam.
Mhitimu Bi. Elizabeth Mnzava akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM,
Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) baada ya kufanya vizuri katika masomo yake.
Sehemu ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa
Fedha-IFM, wakinyanyua juu kofia zao kwa furaha kuashiria kumaliza
sehemu ya safari yao ya kimasomo, baada ya kutunukiwa vyeti na shahada
nyingine mbalimbali, katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es
Salaam.
Mmoja wa wahitimu ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara
moja akionesha furaha isiyo kifani baada ya kutunukiwa Shahada yake
baada ya kuhitimu masomo katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Jijini
Dar es Salaam, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Sehemu ya wahitimu wa Mahafali ya
43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, wakinyanyua kofia zao juu kwa
furaha baada ya kutunukiwa shahada zao wakati wa mahafali hayo
yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewaonya
wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kuacha tamaa ya kutaka
kupata mali za haraka haraka na kutojihusisha na vitendo vya rushwa na
ufisadi wawapo kazini ili waweze kuisadia nchi kufikia maendeleo ya
haraka.
Dokta Mpango aliyasema hayo
wakati akiwatunuku vyeti vya kozi mbalimbali wahitimu 2692 wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha IFM, wakati wa mahafali ya 43 ya Chuo hicho
yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa moja ya changamoto
zinazoikabili jamii hivi sasa ni mmomonyoko wa maadili katika utumishi
wa Umma hali iliyosababishwa na suala la rushwa na ufisadi kuota mizizi
na kuwa tatizo kubwa katika jamii.
“Katika miaka ya karibuni
kumekuwa na matatizo mengi ya matumizi mabaya ya fedha za umma ikiwemo
watumishi hewa, wanafunzi hewa na pembejeo hewa, nawataka wahitimu
mkafanyekazi zenu kwa kuzingatia maadili na kuepuka tabia ya kutaka
utajiri wa harakaharaka” Alisisitiza Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango alitumia fursa hiyo
pia kuelezea mafanikio makubwa yaliofikiwa nchini katika sekta ya fedha
katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa kuimarisha upatikanaji
wa huduma, mikopo ya mitaji ya kuwekeza katika Sekta mbalimbali na
kuhakikisha kuwa sekta hiyo inabaki imara.
Alisema kuwa kutokana na hatua
hizo, idadi ya taasisi za fedha imeongezeka kutoka 31 zilizokuwepo mwaka
1999 hadi kufikia 67 Novemba mwaka 2017 huku taasisi hizo zikiwafikia
watu wengi zaidi hadi pembezoni mwa miji hata vijijini.
“Sekta ya Bima nayo imepiga hatua
ambapo kampuni zilizosajiliwa zimefika 31, wakala wa bima 124 kutoka
wakala 1 iliyokuwepo miaka ya 70 huku ukwasi katika kampuni hizo
ukiongezeka kutoka asilimia 47.1 mwezo Juni 2016 hadi kufikia asilimia
49.8 mwezi Juni, 2017.
Alisema kuwa licha ya mafanikio
hayo, taasisi za fedha zimekuwa zikiathiriwa na uwepo wa mikopo chechefu
iliyoongezeka hadi kufikia asilimia 10.74 mwaka huu ikilinganishwa na
asilimia 9.07 mwaka 2016 na kutoa wito kwa wahitimu hao kubuni mikakati
ya kukabiliana na changamoto kama hizo na kuendeleza mafanikio
yaliyopatikana kwa kuzingatia mahitaji ya Taifa ili kuondokana na
umasikini.
Aidha, Dokta Mpango alisema kuwa
Serikali itaendelea kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wenye
uhitaji ambapo katika Bajeti ya Mwaka huu, imepanga kutumia zaidi ya
shilingi bilioni 427.54 kwa kazi hiyo kwa kuwalipia ada na gharama
nyingine za masomo wanafunzi 122,623.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha
Usimamizi wa Fedha IFM Prof. Lettice Rutashobya ameiomba Serikali
kukisaidia Chuo hicho kwa kukipatia fedha ili kiweze kujiimarisha na
kuendelea kutoa taaluma bora ya masuala ya fedha, uhasibu, bima, TEHAMA
na Hifadhi ya jamii huku Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tadeo Satta akisema
kuwa chuo hicho kimejipanga kujenga kampasi mkoani Pwani na mkoani
Dodoma ikiwa ni mikakati ya kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi
zaidi.
Aidha viongozi hao wa Chuo cha
IFM waliiomba Serikali kutenga shilingi bilioni 2 kila mwaka katika
Bajeti ya Serikali ili waweze kuzitumia kujenga kampasi hizo mbili, moja
katika eneo la Msata mkoani Pwani na nyingine inayotarajiwa kujengwa
mkoani Dodoma.
“Katika hatua za awali wakati
tunataka kutumia eneo la ekari 50 tulilolipata mkoani Dodoma, Chuo
kimepanga kuanza kutoa mafunzo ya shahada ya uzamili katika fani ya
fedha na uwekezaji kwa kutumia miundobinu ya Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini mkoani Dodoma.
Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM
kilianzishwa mwaka 1972 kikianza na kozi mbili na kutoa wanafunzi 75
lakini hivi sasa chuo hicho kinatoa kozi 23 ambapo mwaka huu wahitimu
2692 wamemaliza masomo yao.










0 Comments