Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Presha ya Macho wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Neema Daniel Kanyaro (kulia) akimfanyia
upasuaji mgonjwa mwenye tatizo la presha ya macho kwa kushirikiana na
madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Mtakatifu Thomas ya Uingereza.
Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Macho, Dkt. Pouya Alaghband na
Profesa Lim Sheng kutoka hospitali ya Mtakatifu Thomas.
Madaktari bingwa wa macho wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
kushirikiana na madaktari bingwa wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji
kwa mgonjwa mwenye tatizo la presha ya macho.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Presha ya Macho wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Neema Daniel Kanyaro akimwandaa mgonjwa
mwingine kabla ya kuanza kufanyia upasuaji wa macho leo.
Sehemu ya jicho ikionekana katika ‘screen’ wakati upasuaji wa
presha ya jicho ukiendelea kufanywa na madaktari bingwa kutoka Hospitali
ya Mtakatifu Thomas ya Uingereza kwa kushirikiana na madaktari wabobezi
wa Muhimbili.
Dar es salaam
Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH-
kwa kushirikiana na Hospitali ya Mtakatifu Thomas ya Uingereza inafanya
upasuaji kwa wagonjwa wenye matizo ya pressure macho zoezi lililoanza
leo na linataraji kukamalizika Disemba 7 mwaka huu.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa
macho na pressure ya jicho katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Neema
Kanyaro amesema jumla ya wagonjwa 23 watafanyiwa upasuaji huo ambapo
kati ya hao watatu ni watoto.
Kwa mujibu wa Dkt. Neema upasuaji
huo unafanyika kwa kumuwekea mgonjwa kifaa maalum cha kupunguza pressure
ya jicho ambapo kifaa hicho kinasaidia kupunguza maji kwenye jicho.
‘’ Jicho linapata pressure
kwasababu maji yanakuwa mengi kwenye jicho kwahiyo kifaa hicho (Implant)
kitawekwa kwa mgonjwa ili kupunguza maji kwenye jicho, pia kifaa hiki
kinagharimu kati ya Dola 500 hadi Dola 1,000 .’’ Amesema Dkt. Neema.
Ametaja dalili ya pressure ya
macho kwa watu wazima ni kutokuona ambapo kwa watoto jicho linakuwa
kubwa , jicho linatoa machozi na pia mboni ya jicho kuwa nyeupe.
Aidha Dkt. Huyo ametoa ushauri kwa
watu wazima wenye umri kuanzia miaka 40 kujenga utamaduni wa kufanya
uchunguzi wa pressure ya macho angalau mara moja kwa mwaka ili kuweza
kugundua tatizo mapema na kupata tiba kwa wakati.




0 Comments