Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony
Mavunde ameyataka makampuni,viwanda na Taasisi mbalimbali nchini kusaidia
kufadhili mchezo wa Karate nchini ambao umeanza kukua kwa kasi hivi sasa.
Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifungua mashindano ya
kitaifa ya Karate katika ukumbi wa Kilimani Dodoma yanayojumuisha Timu za
Karate kutoka Mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya timu waalikwa kutoka Kenya.
“Wafadhili wengi hivi sasa wameweka nguvi kubwa katika kusaidia
michezo ya mpira miguu,pete,wavu na kikapu,ni muda sasa muafaka sasa
kuangalia aina mingine ya michezo kama huu wa karate ambao unaweza kutuletea
sifa katika medani za kimataifa”Amesema Mavunde.
Awali, akimkaribisha Mavunde, Kiongozi wa Karate nchini Kitte
Mfilinge amemuomba Waziri Mavunde kusaidia kuutangaza na kuukuza mchezo huu kwa
kushirikiana na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili upate uzito unaostahili
kama ilivyo michezo mingine.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana
na Ajira Anthony Mavunde akifungua mashindano ya Karate.





0 Comments