Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifafanua jambo mbele ya wanakijiji wa kijiji
cha Mbuluni wilayani Mkinga mkoani Tanga (hawapo pichani) katika mkutano wa
hadhara.
Sehemu
ya wakazi wa kijiji cha Mtindiro kilichopo Muheza mkoani Tanga wakifuatilia
hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo
pichani)
Na
Greyson Mwase, Tanga
Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
amezitaka kampuni za Derm Electric,
Njarita, Agwilla na Radi Services kutoa
maelezo kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ya kutokuendelea na kazi
katika maeneo yao ya miradi wakati walikwishalipwa malipo ya awali na Serikali.
Mgalu
alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki tarehe 16 Desemba, 2017 alipofanya kikao na
watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)- Ofisi ya Tanga baada ya
kubaini wakandarasi hao hawapo katika maeneo hayo ya kazi na kutohudhuria kikao
hicho kama alivyoagiza.
Kikao
hicho kilishirikisha pia watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA)
Alisema
kitendo cha wakandarasi kutokuwepo
katika maeneo yao ya kazi na kutohudhuria kikao kama ilivyoagizwa kinakwamisha
utekelezaji wa miradi na hivyo kuutaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
kujulisha kampuni husika kuandika maelezo ya kutokuwepo kwenye maeneo ya kazi na kukwamisha juhudi za Serikali katika usambazaji wa umeme vijijini.
“
Kama Serikali tumeweka mikakati ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2019- 2021 vijiji
vyote nchini vinafikiwa na huduma ya umeme, sasa inapotokea baadhi ya
wakandarasi wanakwamisha juhudi hizi
wakati wamekwishalipwa na Serikali ni lazima Serikali iwawajibishe kulingana na
sheria na kanuni za nchi,” alisema Mgalu.
Mgalu
aliendelea kuwataka wakandarasi wote
nchini kuwepo katika maeneo yao ya kazi
na kukamilisha miradi yao kwa wakati, na kusisitiza kuwa serikali haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayefanya
kazi katika kiwango cha chini.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Mgalu aliitaka TANESCO kuwa wabunifu kwenye
ukusanyaji wa madeni na kukamilisha
zoezi la uhakiki wa wateja mara moja ili
kukabiliana na changamoto ya upotevu wa mapato ya shirika hilo.
Alisema
ni jukumu la TANESCO kujiendesha kwa faida kupitia mapato yake na kazi ya
Serikali ni kulipa nguvu shirika hilo kwa miradi mikubwa inayohitaji fedha
nyingi.
Wakati huo huo,
akizungumza katika mikutano tofauti katika kijiji cha Zangibari kilichopo
wilayani Mkinga na katika vijiji vya Mlingano,
Mtindiro, Mpapayu vilivyopo katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Naibu
Waziri Mgalu alielekeza wakati wa utekelezaji wa miradi, Wakala wa Nishati
Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kuhakikisha taasisi, shule, nyumba za ibada,
hospitali zinapata umeme.
Aidha alipongeza wananchi wengi katika vijiji vya Zangibari wilayani Mkinga
na Mpapayu wilayani Muheza mkoani Tanga walioonyesha mwitikio mkubwa wa kuunganisha
mfumo wa umeme ( wiring) kwenye nyumba zao na kuwataka ambao hawajaunganisha
mfumo wa umeme kufanya mara moja kwa ajili ya neema kubwa ya umeme.
Alisema
kwa wale ambao wana nyumba ndogo wanaweza kuwekewa kifaa maalum cha Umeme Tayari
(UMETA) na kuanza kufaidi huduma ya umeme.
Akielezea
mikakati ya serikali katika uboreshaji wa upatikanaji wa umeme wa uhakika na
kwa gharama nafuu, Mgalu alisema kuwa serikali kupitia REA Awamu ya Tatu inasambaza umeme katika vijiji vyote nchini ambapo ifikapo mwaka 2019 karibia vijiji vyote
vitakuwa na umeme wa uhakika.
Aliendelea
kuelezea mikakati mingine kuwa ni pamoja na matumizi ya nishati jadidifu kama vile jua hususan katika maeneo
yasiyofikiwa na umeme kutoka Gridi ya Taifa, ujenzi wa mradi
wa kuzalisha umeme kwa kutumia
maporomoko ya maji ya Mto Rufiji wa
Stieglers Gorge na mradi wa kuzalisha
umeme kwa kutumia gesi asilia wa
Kinyerezi I na Kinyerezi II.


0 Comments