Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (katikati)
akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Taifa
ya Saadani na Mwakilishi wa Mkuu wa
Hifadhi za Taifa, Vitalis Kuluka huku akishirikiana kuonesha eneo hilo na
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,Erica Yigella ( wa pili kulia) mahali
kilipo Kitongoji cha Uvinje ambapo wakazi wa eneo hilo wamegoma kuhama ndani ya
hifadhi hiyo na wakati Naibu Waziri huyo
alipotembelea hifadhi hiyo jana.
Wa kwanza kulia ni Afisa Wanyamapori,
Godfrey Maro na Wa kwanza kushoto ni
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Stephano Msumi na pande wa kulia nyuma ya
Katibu Tawala ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu .
(Picha na Lusungu Helela-MNRT
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia
) akizungumza na Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Saadani , Stephano Msumi (
katikati) wakati Naibu Waziri huyo
alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali
zinazoikabili . Wa
kwanza kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Erica Yigella, Wa kwanza
kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Vitalis
Kuluka, wa tatu kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa
Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu .
(Picha na Lusungu
Helela-MNRT
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga akizungumza
jana na
Wananchi wa Kitongoji cha Uvinje
ambao wamegoma kuhama ndani ya hifadhi
hiyo, wakati Naibu Waziri huyo
alipotembelea kwa ajili ya kuzungumza nao ili kujua ukubwa tatizo la mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 10
sasa . (Picha na Lusungu Helela-MNRT
Bango lililopo katika geti
la Gama linalokuelekeza sheria na
taratibu ukiwa unaingia katika Hifadhi
ya Taifa ya Saadani iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga ( kushoto ) akipatiwa maelezo na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani , Stephano Msumi ( katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea
hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili .Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa,
Vitalis Kuluka, nyuma
ya Mhifadhi wa Saadani ni Msaidizi wa
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,
Fredrick Mofulu .
(Picha na Lusungu Helela
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga ( mbele ) akiwa
na baadhi ya viongozi wa Hifadhi za Taifa
pamoja kamati ya ulinzi na
usalama kutoka Wilayani Bagamoyo akiongoza kwenda kuangalia sehemu
kunakofanyika utalii wa boti katika
Hifadhi ya Taifa ya Saadani wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea
hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili .
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kulia)
akipatiwa maelezo na Msaidizi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,
Fredrick Mofulu ( wali kushoto) kuhusiana na sehemu kunakofanyika utalii wa boti
katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani
. Wengine ni
baadhi ya viongozi wa Hifadhi za
Taifa pamoja na kamati ya ulinzi kutoka
Wilayani Bagamoyo .
(Picha na Lusungu Helela
Wananchi wa Kitongoji
cha Uvinje kilichomo ndani Hifadhi
ya Taifa ya Saadani iliyopo wilayani Bagamoyo Mkoani wa Pwani wamesema hawapo tayari kuhama wala kulipwa fidia ili kupisha hifadhi hiyo.
Kitongoji
hicho, ambacho ni kati ya vitongoji nane vya Kijiji cha Saadani, kilitakiwa
kiondolewe tangu mwaka 2005 baada ya hifadhi hiyo kupandishwa daraja kutoka
pori la akiba na kuwa hifadhi kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Namba 281 la
Septemba 16, 2005.
Akizungumza
mbele ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya
ya Bagamoyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati alipofanya ziara jana katika kijiji hicho aliwambia wananchi hao kuwa lengo
la ziara yake ni kutaka kuwasikiliza juu mgogoro huo na sio kuwahamisha.
‘Mimi
ni mgeni kidogo kwenye Wizara hii, Nimekuja kuangalia sio kuwahamisha kwa kuwa sijui eneo hili lina
ukubwa kiasi na lina kaya ngapi lakini
nimekuja kutembelea hifadhi na maeneo yote yenye changamoto. ‘’ alisema
Alisema amefika kwa ajili ya kuwasikiliza ili aweze kujua jinsi mgogoro
ulivyo kwa sababu hakutaka kusikia
upande mmoja wa TANAPA pekee.
Naye , Kaimu Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Hassan Akida alisema wakazi wa eneo hilo hawapo tayari kuhama na
wala kulipwa fidia kwa vile ni ardhi yao
tokea enzi za mababu zao.’
‘Tumesema hapa ndo kwetu mnataka
kutuhamisha mtupeleke wapi wakati sisi tumezoea maisha yetu hapa’’ alisema
Akida.








0 Comments