Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akitoa maelekezo kwa Benki nchini
kuangalia namna ya kupunguza riba kwa wakopaji na pia kufuata vigezo stahiki
kwa mkopaji ili kuondoa mikopo chechefu wakati wa mkutano kati yake na
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu Hali ya uchumi na
utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 ambapo alitoa agizo kwa
vyombo vya ulinzi kuwakamata wanaowalazimisha watanzania kufanya malipo kwa
Dola badala ya Shilingi, mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mbele) akiwa katika Mkutano na
waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali
kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaabani (kushoto) akizungumza
na wadau waliohudhuria Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na waandishi wa habari katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kulia.
Maafisa Waandamizi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifurahia jambo wakati Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliangazia suala la hali ya Uchumi na
kubainisha kuwa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki,
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa na Afisa Mwandamizi wa Wizara
hiyo Bw. John Sausi wakizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na
Waandishi wa Habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali
kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.






0 Comments