Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akikagua gwaride.
Kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akiteta jambo na Mshauri Jeshi la Akiba Gairo, Major Balitoga (kushoto kwake) pembeni ni Diwani wa Kata ya Rubeho, Mhe. Mhe. Digwagwala (wa kwanza kulia).
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
Mshauri Jeshi la Akiba Gairo, Major Balitoga akitoa machache mbele ya mgeni rasmi.
Diwani wa Kata ya Rubeho Mhe. Digwagwala akitoa shukrani zake za pekee kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kwa kuweza kuendesha mafunzo katika Kata yake.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Rubeho akikagua gwaride.
Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakiwa katika gwaride la ukakamavu mbele ya mgeni rasmi.
Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakiwa katika gwaride la ukakamavu mbele ya mgeni rasmi.
Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akitoa hotuba yake.
Brass Bendi wakitumbuiza katika hafla hiyo ya kuhitimisha mafunzo ya mgambo yaliyofanyika katika kata ya Rubeho.
Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo wakipita mbele ya mgeni rasmi kwa gwaride la kutoa heshima.
Na Kajunason/MMG.
Mkuu wa wilaya ya Gairo,
Siriel Shaidi Mchembe amewataka wahitimu wa mafunzo ya mgambo kukiishi
kiapo cha utii kwa matendo na si maneno.
Hayo
ameyazungumza leo Disemba 16, 2017 wakati wa hafla ya kuhitimisha
mafunzo ya mgambo ambayo yalifanyika katika Kata ya Rubeho halmashauri
ya wilaya ya Gairo ambapo mgeni rasmi aliwaasa wahitimu kutii yale yote
waliyofundishwa ili kujenga uchumi wa Taifa.
Katika
hotuba yake Mhe. Mchembe aliongeza kuwa mgambo wanapaswa kutumia elimu
waliyoipata ili kuinua uchumi wao na jamii inayowazunguka bila kuwaonea
au kuwatesa wananchi.
"Nawaombeni sana ndugu
zangu mafunzo mliyoyapata ni muhimu sana katika taifa letu ni vyema sasa
na nyie mkayaishi yale yote mliyofundishwa kwa kipindi cha miezi mitatu
mliyoshiriki," alisema Mhe. Mchembe.
Aliongeza
kuwa ni vyema mgambo wakawa mabalozi wema wa amani na si wao wawe
mstari wa mbele katika vitendo vya rushwa, unyanyasaji wa wananchi na
kuepuka kujihusisha kwenye uharifu kwa kukodisha magwanda yao.
Mhe.
Mchembe aliwataka viongozi wa wilaya kufanya usaili tena kwa wale
mgambo wote ambao wameshapitisha miaka 10 ili waweze kurudi kupata
mafunzo zaidi.
"Kazi hii ya mgambo inahitaji
kuendelea kujifunza mara kwa mara hivyo nawaomba viongozi wote fanyeni
upya usaili wale wote ambao muda wa miaka 10 umepita warudie katika
mafunzo waweze kuongeza ujuzi zaidi," alisema Mhe. Mchembe.
Alimalizia
kwa kuwataka viongozi wa wilaya kuwahamasisha akinamama kujitokeza
zaidi katika mafunzo ya mgambo maana idadi yao imeonekana kuwa ni ndogo
sana ukilinganisha na wanaume ambao wao wamekuwa mstari wa mbele katika
kujitokeza.
Mafunzo hayo ya miezi mitatu
yalihitimishwa Disemba 13, 2017 yalisimamiwa na Mshauri Jeshi la Akiba
Gairo, Major Balitoga kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama
Wilaya ambapo jumla ya wahitimu 101 ambapo asilimia 11 tu walikuwa ni
wanawake.
Wahudhuriaji hafla hiyo walikuwa ni
Diwani wa Kata ya Rubeho Mhe. Digwagwala, Mtendaji wa Kata, Wenyeviti wa
vijiji, viongozi wa dini, wazee maarufu na wananchi zaidi ya 200
walishiriki maadhimisho hayo.









0 Comments