Mke wa Tito Machibya Maarufu kwa jina la Nabii Tito, Agnes Miri (36), ameweka kambi Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Dodoma, akishinikiza mume wake atolewe kwani amekuwa akiishi maisha magumu.
Nabii huyo ambaye jana alijaribu kujiua kwa kujikata na wembe tumboni na kushonwa nyuzi 25, akiwa chini ya Jeshi la Polisi bado anashikiliwa na jeshi hilo.
Akiwa na watoto wake watatu katika viunga vya polisi, mke wa nabii huyo ambaye amekuwa akionekana na mume wake wakicheza muziki na kunywa pombe, ameiambia Mtanzania Digital, anaomba jeshi hilo limwachie mume wake kwani maisha yamekuwa magumu kwake.
Amesema yeye na watoto wake wanaumwa ugonjwa wa kuhara na kutapika ambapo kutokana na mume wake ambaye ndiyo mwangalizi wa familia kushikwa na polisi hana mtu wa kumsaidia.


0 Comments