Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb), katikati, akiwa katika
kikao na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya, wa pili kutoka
kushoto.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb), akiwa katika kikao na
balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya, wa pili kutoka kushoto.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni
(mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) ameiomba Serikali ya India kuendelea
kuwajengea uwezo watumishi wa umma nchini.
Mhe.
Mkuchika amesema hayo leo katika kikao na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep
Arya ambaye ameahidi nchi yake kuendelea
kutoa ufadhili katika fani mbalimbali kwa Watanzania.
“Watumishi
kujengewa uwezo katika maeneo yanayohusu
TEHAMA, Afya na Viwanda yatasaidia sana nchi yetu” Mhe. Mkuchika amesema
mpango wa maendeleo wa Taifa wa 2025 unatilia mkazo viwanda ili kuleta
mabadiliko ya uchumi na jamii.
Balozi
Sandeep Arya kwa upande wake amesema nchi yake imepanga kwa siku za usoni
kuendesha warsha na mafunzo kwa njia ya kieletroniki (e-corses) ambapo katika eneo
la Afya amesema ili kujenga uwezo zaidi utafanyika utaratibu wa kubadilishana
wataalam wa afya kati ya nchi yake na Tanzania.
“Tunapanga
pia kuleta watalaam na kutoa mafunzo hapa Tanzania” Balozi Arya amesema na
kuongeza kwa mwaka huu 2018 wameongeza mafunzo kuhusu vita dhidi ya madawa ya
kulevya ikiwamo matumizi na usafirishaji wake.
Imetolewa
na
Florence
Lawrence
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano-UTUMISHI
05.01.2018



0 Comments