Mheshimiwa
Job Ndugai (Mb) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameielekeza Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kukutana ili kuchunguza na kujadili kauli
ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka, inayodhalilisha
Bunge.
Mheshimiwa
Spika amechukua hatua hiyo kufuatia kauli zilizonukuliwa katika mitandao ya
kijamii kwa lugha za kimasai, kiswahili na kiiengereza, zikiashiria kejeli na
dharau kwa Bunge na hivyo ameelekeza kuwa wakati wa kuchunguza suala hilo
Kamati imuite na kumuhoji ili kubaini ukweli na dhamira ya kauli hizo na kutoa
mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.
Imetolewa
na: Ofisi ya Spika
S.L.P.
941
DODOMA
09
Januari 2018

0 Comments