§
Tanzania yajipanga kutetea ushindi ilioupata msimu uliopita
§
Wanafunzi wakereketwa wa Sayansi na Teknolojia kuonyeshana umwamba
Msimu
wa saba wa tuzo maarufu barani Afrika kwa wanafunzi wapenzi wa masomo
ya Sayansi na Teknolojia - DStv Eutelsat Star Awards umezinduliwa rasmi
ambapo Tanzania ambayo ilishika nafasi ya pili katika tuzo za
mwaka jana kupitia mwanafunzi Davids Bwana, inatarajia kuongeza nguvu
na hatimaye kuibuka kidekea.
Kama
ilivyokuwa siku za nyuma, tuzo hizo zinahusisha uandishi wa insha maalum
au kuandaa bango vyenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan
Setelait. Wanafunzi wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka
14 – 19 wanaruhusiwa kushiriki kinyang’anyiro hicho kitakachoendelea
adi mwishoni mwa mwezi Februari 2018
Kwa
miaka sita mfululizo, Tuzo hizi zimekuwa chachu kubwa kwa vijana wenye
ari ya kuwa wanasayansi huku zikiangazia ni jinsi gani sayansi ya
setelait inavyoweza kubadilisha
maendelea, uchmi, na maisha kwa ujumla ya watu wote ulimwenguli.
Akizungumzia tuzo hizo na jinsi walivyojipanga
kuhakikisha kuwa tanzania inafanya vizuri, Mkurugenzi wa Multichoice
Tanzania Maharage Chaned amesema kuwa mwaka jana takriban shule 50
kutoka tanzania zilishiriki na jumla ya wanafunzi Zaidi
ya 200. Kwa mwaka huu amesema wanawasiliana na shule nyingi zaidi ili
kuhakikisha kuwa washiriki wanaongezeka.
“Tumejipanga na tunawasiliana na shule nyingi zaidi
kote nchini ili kuhakikisha kuwa siyo tu tunapata washiriki wengi, bali
tunapata kazi nzuri pia zenye kiwango cha juu cha kuweza kushindana na
wanafunzi wan chi nyingine” alisema Maharage
na kuongeza kuwa idara ya Uhusiano ya MultiChoice ndiyo inayoratibu
zoezi hilo na hivi sasa tayari takriban shule 50 kutoka mikoa mbalimbali
zimeshajulishwa moja kwa moja. Hata hivyo alisema maelezo yote yapo
mitandaoni hivyo wanafunzi wote wenye sifa wanaweza
kushiriki. Kuanzia leo tutaanza pia kutoa matangazo sehemu mbalimbali
ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii ili kuhamasisha ushiriki mkubwa.
Amewataka walimu na wazazi kuwapa moyo na ari
wanafunzi wao ili washiriki katika tuzo hizi ambazo ni kubwa na za aina
yake hapa barani Afrika.
Kwa
mwaka huu, washindani watatakiwa kuandika insha au kubuni bango kuhusu
manufaa yaliyoletwa na uvumbuzi wa setelaiti katika maisha ya kila siku
hapa ulimwenguni na ni jinsi
gani setelait imekuwa kama kiungo muhimu kwa shughuli zote
zinazofanyika kote duniani.
Kama kawaida tuzo hizi zina zawadi kabambe ambapo mshindi wa Insha atapata fursa ya kuzuru kituo cha Eutelsat
nchini Ufaransa na pia kwenda Guiana kushuhudia mubashara urushwaji wa setelait angani.
Mshindi
wa bango atajishindia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini na
kutembelea kituo cha anga cha nchi
hiyo na pia makao makuu ya MultiChoice Africa akiwa kama mgeni maalum.
Shule zitakazotoa washindi hao zitapata zawadi ya kufungia huduma ya
DStv bure.
Insha
pamoja na mabango hayo hupitiwa na timu ya watahini wenye uzoefu mkubwa
katika hatua mbili. Hatua ya
kwanza ni katika kila nchi inayoshiriki ambamba kila nchi huwasilisha
mshindi wa Insha na mshindi wa Bango. Hawa wawili huingia kwenye
kinyang’anyiro na washindi kutoka mataifa mengine kote barani afrika.
Washiriki wote wanaweza kupata fomu za ushiriki kutoka ofisi zote za Multichoice au mtandaoni kupitia
www.dstvstarawards.com.
Lugha inayotumika
kwa tuzo hizo ni Kiingereza na kazi zote zitakazowasilishwa
zitatathminiwa kulingana na vigezo mbalimbali ikiwemo ubunifu, usahihi
wa maelezo na uhalisia. Pia kuwa mara ya kwanza washiriki wote wanaweza
kutoa maoni na kuwasiliana kupitia ukurasa maalum wa
facebook.
Taarifa zote kuhusu vigezo, zawadi na nyinginezo zinapatikana katika
tovuti maalum ya tuzo hizo ambayo ni: http://www.dstvstarawards.com/ about.html

0 Comments