Mbunge wa Jimbo la Dodoma
Mjini Anthony Mavunde amewataka askari wa kike wa Jeshi la Polisi
mkoani Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo mkoani hapo kwa
kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na uchumi wa
viwanda.
Mavunde
ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Chama cha Polisi Wanawake
katika semina fupi aliyoiandaa katika Bwalo la Polisi-Dodoma kwa lengo
la kuwapa Askari Polisi elimu juu ya masuala ya UJASIRIAMALI na
UWEKEZAJI.
“Najua jukumu
lenu la msingi ni Ulinzi wa Mali na Raia,lakini si vibaya pia mkautumia
muda wenu wa ziada kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la
kuwaongezea kipato”amesema Mavunde
Naye,Kiongozi
wa mtandao wa Askari Polisi wanawake Mkoa wa Dodoma SP Hiki amemshukuru
Mbunge Mavunde kwa kuona haja na umuhimu wa kukutana na Askari hao na
kufanikisha semina hiyo ambayo imehusisha wataalamu kutoka SIDO,Mifuko
ya Uwezeshwaji na Wataalamu kutoka Manispaa ya Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza katika semina fupi ya Chama cha Polisi Wanawake.
washiriki wa semina.





0 Comments