Meneja
wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi kwa niaba
ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa na Kamishna wa Fedha,
Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji
wakikabidhiana hati ya makabidhiano ya nyumba baada ya kukabidhi nyumba
63 kwa Jeshi la Uhamiaji.
Picha
ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya
makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite
Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi
zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za
gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.

Wafanyakazi
na uongozi wa Jeshi la Uhamiaji wakiwa wameshika mfano wa ufunguo baada
ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite
Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi
zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za
gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) leo limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa
kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa
Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.
Mradi
huu ambao ujenzi wake ulianza Desemba 2016 una ukubwa wa ekari 234 na
ni moja ya sehemu ya mji uliopangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria
na kanuni za mipango miji na utajengwa katika awamu tatu. Nyumba hizi 63
ambazo zimeshakamilika na kuanza kukaliwa zinakabidhiwa leo kwa Idara
ya Uhamiaji.
Makabidhiano
haya yamefanywa na Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Ndugu
Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC na Kamishna wa
Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Makabidhiano
haya yanafanyika baada ya ahadi ya Shirika la Nyumba kwa Mheshimiwa
Rais John Pombe Magufuli ya kujenga nyumba makao makuu ya nchi Dodoma.
Katika
uzinduzi wa nyumba hizi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC alimhakikishia Mh. Rais
kwamba nyumba hizi zimekamilika na ziko tayari kwa kukaliwa.
Leo
ni siku ya furaha kuona kwamba NHC inakabidhi nyumba kwa Uhamiaji
ambaye ni mmoja wa wanunuzi wakubwa wa nyumba katika mradi huu.
Nyumba hizi ni bora kabisa zimejengwa kwa ustadi mkubwa. Ni wito wetu kwamba nyumba hizi watazitunza ikiwa na mazingira yake.
Mradi huu wa nyumba 300 ikiwa 150 zimekamilika ni kati ya miradi mingi ambayo NHC inatekeleza.

0 Comments