Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo (katikati) akipokea Taarifa ya Ujenzi wa miundombinu ya Afya
katika Kitoa cha Afya Karume kilichopo Wilayani Rombo.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati)
akitoa maelekezo katika kituo cha Afya Mikumi baada ya kupokea Taarifa ya
Ujenzi.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiendelea
na Ukaguzi katika kituo cha Afya Mikumi Wilayani Rombo.
Hii ni baadhi
ya muonekano wa majengo yanayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Mikumi-Rombo.
Muonekano wa majengo yanayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Mikumi-Rombo.
Nteghenjwa
Hosseah, TAMISEMI.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo
ametoa mwezi mmoja kwa Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kukamilisha
ujenzi wa kituo cha Afya Karume ambao uko nyuma ya wakati kwa mujibu wa ratiba
ya ujenzi wa vituo hivyo ambao unaendelea kote Nchini.
Wakati akikagua Kituo hicho Waziri Jafo amesikitishwa na
kasi ndogo ya Ujenzi wa Kituo hicho unaopelekea kuzorotesha malengo ya Serikali
ambao umejikita katika Utoaji wa huduma bora za Afya na za wakati kwa Wananchi.
Waziri Jafo alisema Kituo hiki kimepokea Fedha
za ujenzi tangu mwezi Septemba, 2017 na kilitakiwa kiwe kimekamilisha
ujenzi huu mwishoni mwa Disemba 2017, lakini mpaka sasa ujenzi ndio
umefikia kwenye hatua ya Kuezeka.
“Nataka mkajifunze kwa wenzenu ambao walipokea Fedha za Ujenzi
sawa na nyie na wamekwishajenga Nyumba ya Mtumishi, Jengo la Maabara, Chumba
cha Upasuaji, Wodi ya Kina Mama, Chumba cha kuhifadhia maiti, pamoja na
kichomea Taka” Alisema Jafo.
Aliongeza kuwa Kwenye baadhi ya vituo vya Afya wamejitahidi
kutumia kwa umakini Fedha hizo na kuongeza na Njia ya Kutembelea Wagonjwa,
wodi ya watoto na kufanya Ukarabati majengo ya zamani kwa gharama hiyo hiyo ya
Tsh Mil 500 ambazo nyie mpaka sasa hamjakamilisha majengo yenu”
Alimalizia kuwa ifikapo Tar. 25 Februari 2018 ujenzi
wa miundombinu hii ya kituo cha Afya iwe imekamilika na nipate Taarifa kutoka
kwa Mkuu wa Wilaya na ikiwezekana nitapita mwenyewe kuhakiki ubora wake.





0 Comments