Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwasili katika Hospital ya Wilaya ya Hai
kukagua ujenzi wa miundombinu ya Afya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kulia)akikagua ujenzi wa Duka la Dawa linaloendelea
kujengwa katika Hospital ya Wilaya ya Hai.
Hii ndiyo Hospital ya Wilaya ya Hai ambayo mpaka sasa haijafunga
mfumo wa Uendeshaji na Usimamizi wa Kutolea huduma za Afya - GoTHoMIS.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amekasirishwa na uongozi wa
hospital ya Wilaya ya Hai kwankushindwa kutumia mfumo wa Uendeshaji na
Usimamizi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya.
(GoTHoMIS).
Waziri Jafo akiwa ziarani Katika
Wilaya hiyo kukagua ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Hospital ya Wilaya
alihoji endapo Hospital hiyo imeanza kutumia mfumo wa GoTHoMIS
katika uendreshaji na usimamizi wa huduma za Afya ikiwa ni agizo alilolitoa
miezi michache iliyopita wakati alipotembelea Hospital hiyo.
Majibu aliyoyapata katika Hospital
hiyo hayakumridhisha ambapo Uongozi wa Hospital na Wilaya hiyo ulidai
kutokua na mtaalam wa mifumo ya Tehama wa kusimamia usimikaji wa Mfumo
ilihali vifaa vyote kama vile Computer kwa ajili ya matumizi ya mfumo
vimekwishafika tayari kuanza kutumika.
“Haiwezekani Halmashauri za
pembezoni watumie mfumo huu katika uendeshaji wa shughuli zao na nyie wa Mjini
kabisa mpaka leo mnasingizia eti hamna mtaalamu, mlishindwa kutafuta hata
kutoka katika Halmashauri za Jirani au mna vitu mnavifanya na mnaona
mfumo ukianza kutumika hamtaweza kuendelea kufanya tena hayo mnayoyaficha ”
Aliongeza kuwa mapato mnayokusanya
katika Hospital hii hayaridhishi ukilinganisha na Idadi ya wagonjwa wanaokuja
kutibiwa kwa siku na mkianza kutumia Mfumo huu utaonyesha mapato sahihi ambayo
mnakusanya na hili ndio ninaloona mnalikwepa, sasa ninawapa wiki mbili tu mfumo
huu uwe umeanza kutumika.
Akitoa Taarifa ya Hospital hiyo mganga Mkuu wa
Wilaya hiyo alisema mapato yanayokusanywa kwa mwezi ni zaidi ya Mil. 50 na kwa
kipindi cha Miaka 50 wamekusanya zaidi ya Mil 300 na baada ya kukamilisha
ujenzi wa Duka la Dawa la Hospital hiyo watakusanya Fedha nyingi Zaidi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai
amemuahidi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mhe.Selemani Jafo kuwa mfumo huo utakamilika ndani ya wiki moja na utaanza
kutumika katika kusimamia na kuendesha shughuli za utoaji wa huduma za Afya
katika Hospital ya Wilaya ya Hai.
0 Comments