*Amuagiza CAG kufanya uchunguzi tangu kuanzishwa kwake

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza zao la Kahawa (CDTF) na amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Januari 14, 2018) wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa AMIMZA Coffee Products ya Tanzania, Amir Hamza, baada ya kukutana na wadau wa zao la Kahawa kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao hilo, kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina, mjini Dodoma. Januari 14, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Angalia Video Hapa Chini.↓
0 Comments