Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia vipepeo
katika moja shamba la wafugaji katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana.
Mbali na biashara ya kuuza vipepeo hao nje ya nchi aliwataka wafugaji
hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa
maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira
Asilia Amani
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya pambo
la vipepeo kutoka kwa mmoja wa wafugaji Asina Athumani muda mfupi baada
ya kukagua shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana
ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa
ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea
Hifadhi ya Mazingira Asilia.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisaidia baadhi ya watu
kupanda mlima baada ya kukagua chanzo cha maji cha Mto Zigi ambacho
kipo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani wilayani Muheza mkoa wa
Tanga. Ameiagiza TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo
hilo linalovamiwa na wananchi kwa madai ya kuchimba madini ya dhahabu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya shamba
la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka
wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa
kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya
Mazingira Asilia Amani tofauti na hivi sasa wanapotegemea soko la kuuza
nje ya nchi. Kulia ni Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi
Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho
jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja
na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la
Taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi
Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho
jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja
na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la
Taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi
Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho
jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja
na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la
Taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka
kwa Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kuhusu
kivutio cha utalii cha umbo la asili la ramani ya Afrika alipotembelea
mapango hayo jana Jijini Tanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka
kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos
Santos Silayo kuhusu asali inayozalishwa na Wakala huyo kupitia shamba
la Miti Sao Hill muda mfupi kabla ya kuikabidhi kwa Asha Shaban ambaye
ni dada yake na aliyekuwa mshairi na mwandishi mashuhuri wa riwaya
Shaban Robert alipotembelea makumbusho ya mwandishi huyo Jijini Tanga
jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Asha Shaban
ambaye ni dada yake na Shaban Robert aliyekuwa mshairi na mwandishi
mashuhuri wa riwaya zawadi ya asali inayozalishwa na Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania TFS kupitia shamba la Miti Sao Hill alipotembelea
makumbusho ya mwandishi huyo Jijini Tanga jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo
kukagua Kituo cha Mapango ya Amboni wakati wa ziara yake ya kikazi
Jijini Tanga jana ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja
na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la
Taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo ya namna
ya kupanda miti ya Mitiki kutoka Meneja wa shamba la Miti Longuza
alipotembelea shamba hilo jana wilayani Muheza Mkoani Tanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na
wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi alipotembelea hifadhi hiyo jana
mkoani Tanga.
Na Hamza Temba, WMU, Muheza Tanga
...
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi kinyume cha sheria
"Nimeagiza watu wa TFS wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka, kwasababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwahivo kila siku wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa.
"Kwasababu sisi kazi yetu ni kuhifadhi Maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu, niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa ukifanyika, kwasababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na salama" alisema Dk. Kigwangalla.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huyo, Prof. Dos Santos Silayo alisema pamoja na eneo hilo kwa sasa kuwa linalindwa na askari wa Suma JKT watahakikisha ulinzi unakuwepo muda wote kwa kutekeleza agizo hilo la Waziri la kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu ili askari wawepo katika eneo hilo muda wote.
"Lengo letu ni kuhakikisha kwamba wananchi hawaingii ili tusiwe tunawashtukiza kuwakamata na kwachukulia hatua, lazima tuwe watu wa kuzuia uhalifu usitokee, nia yetu ni kuwa na kituo mara moja kama alivyoelekeza Mhe. Waziri na hili jambo tumelichukua kama maelekezo na tutalitekeleza kwa nguvu kabisa," alisema Prof. Dos Santos Silayo.
Awali Dk. Kigwangalla alitembelea kikundi cha wafugaji wa vipepeo katika Tarafa ya Amani ambao waliiomba Serikali ifungulie vibali vya kusafirisha bidhaa hiyo nje ya nchi, aliahidi kuyafanyia kazi maombi yao huku akiwataka kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani.
Akiwa mkoani Tanga alitembelea pia Kituo cha Mambo ya Kale cha Mapango ya Amboni na kusema Wizara yake itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini viweze kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa.
Katika ziara hiyo ya siku moja mkoani Tanga alitembelea pia shamba la miti ya Mitiki Longuza, Makumbusho ya Shaban Robert na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
0 Comments