Random Posts

Kupandishwa cheo Serikalini Kuzingatia Utendaji

 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi. 
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika kikao kazi na watumishi hao chenye lengo kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi

Waajiri nchini wanatakiwa kuzingatia ufanisi wa utendaji kazi katika hatua za kuwapandisha vyeo watumishi wa umma nchini.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ametoa maelekezo hayo akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe.

Dkt. Ndumbaro amesema lengo la Serikali ni kujenga ufanisi katika Utumishi wa Umma, hivyo suala la upandishwaji vyeo Serikalini lazima lizingatie utendaji kazi wa watumishi wa umma.

Katibu Mkuu Dkt. Ndumbaro amefafanua kuwa watumishi wa umma wakiajiriwa pamoja haina watapandishwa cheo pamoja au muda wa kustaafu watakuwa katika cheo kimoja, bali vyeo vitategemea utendaji kazi wao kati aliyefanya kazi kwa bidii na ambaye hakuwajibika ipasavyo.

Dkt. Ndumbaro amesisitiza waajiri kuzingatia kigezo cha utendaji kazi katika kuwapandisha vyeo watumishi wa umma ili kuimarisha utendaji kazi na kuepuka kuwapandisha vyeo kiholela.

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
 TAREHE 19 FEBRUARI, 2018

Post a Comment

0 Comments