Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt.
Wilbrod Slaa, Balozi Slaa alifika kwenye makazi ya Makamu wa Rais kwa
lengo la kumuaga akiwa tayari kuelekea kwenye kituo chake kipya cha
kazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Balozi
wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto aliyefika nyumbani
kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo
kipya cha kazi, katikati ni Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa Balozi wa Tanzania
nchini Sweden. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt Wilbrod
Slaa (kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin
Ally Mboweto kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar Es Salaam ambapo
Mabalozi hao wawili walifika kwa lengo la kumuga Mhe. Makamu wa Rais.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dkt Wilbrod
Slaa (kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin
Ally Mboweto kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar Es Salaam ambapo
Mabalozi hao wawili walifika kwa lengo la kumuga Mhe. Makamu wa Rais.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Balozi wa Tanzania
nchini Nigeria Mhe. Muhidin Ally Mboweto
pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Wilbrod Peter Slaa leo wakutana
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
kwenye makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga tayari
kwenda kwenye vituo vyao vipya vya kazi.
Mabalozi hao
ambao waliapishwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar Es Salaam
.
Makamu wa
Rais aliwatakia safari njema huko waendapo kwenye vituo vipya vya kazi ambapo
aliwasihi kwenda kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuzingatia maelekezo ya Mhe.
Rais
“Hakikisheni
mnaitangaza nchi yetu vizuri na kuwashawishi wawekezaji ili waweze kuja kwa wingi, nchi yetu ina fursa
za kutosha” alisema Makamu wa Rais.
Kwa upande
wao Mabalozi hao walimuahidi Makamu wa Rais
kuiwakilisha nchi vizuri na kufanya kazi kizalendo.




0 Comments