Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Viongozi wa Dini mara baada ya kuwasili Ikulu Ndogo, Bariadi,
mkoani Simiyu.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasalimia wananchi wa Masanza Kona, Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
(Picha na Ofisi wa Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka
jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli ambao utafaidisha vijiji
vitatu, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphael Chegeni.
(Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka
jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za Viongozi wa Mkoa katika eneo la Nyaumata,
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
(Picha na Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa)
Mbunge
wa Jimbo la Busega Dkt. Raphaele Chegeni akizungumza mbele ya Makamu wa Rais
Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kusalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi
barabarani eneo la Nyashimo kumsalimia Makamu wa Rais ambaye ameanza ziara ya
siku tano mkoani Simiyu.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka
Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuhakikisha kila shule ya sekondari inayojengwa
inajengwa ikiwa na maabara.
Makamu wa
Rais ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi Lamadi wilaya ya Busega mkoani
Simiyu ikiwa siku yake ya kwanza ya ziara ya siku tano mkoani humo.
Makamu wa
Rais ambaye alianza ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa
maji uliopo Kiloleli ambapo mradi huo ukikamilika utasaidia kupatikana kwa maji
safi na salama kwa vijiji vitatu na utagharimu shilingi za kitanzania bilioni
1.6 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 80%.
Makamu wa
Rais aliwapongeza wananchi kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano
katika uwekezaji na uendelezaji wa viwa nda ambapo mpaka sasa kuna viwanda 14
vya usindikaji wa pamba na viwanda vidogo vidogo vya usindikaji mazao 1,035.
“Nawapongeza kwa mkakati wa kuzalisha
bidhaa za afya zinazotokana na pamba na maji ya drip”
Makamu wa
Rais aliwaambia wananchi hao kuwa hadi mwisho wa mwezi huu chupa milioni 2 za
dawa za kuuwa wadudu wanaoshambulia pamba zitakuwa zimesambazwa.
Mwisho
Makamu wa Rais aliwataka Viongozi na Watendaji kushirikiana na wananchi kwani
ushirikiano
Katiak Ziara
hiyo Makamu wa Rais aliweka pia jiwe la msingi la ujenzi wa Nyumba za Viongozi
wa Serikali zilizopo Nyaumata.






0 Comments