Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimkabidhi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi
Kigwangalla kabrasha lenye Andiko la mradi wa REGROW na Mikataba ya
Fedha na utekelezaji wa mradi mara baada ya kuuzindua mradi huo katika
eneo la Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
(picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
(picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa uwekezaji katika miundo mbinu ya mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kabla ya kuzindua mradi wa REGROW.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania (REGROW) ,Kihesa Kilolo mkoani Iringa.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuleta mabadiliko ya dhati katika
sekta ya utalii kwa kuhakikisha inatanua mtandao wa barabara na pia kuweka
mikakati dhabiti ya kuviendeleza vivutio vya utalii viliovyoko kanda ya
Kusini ili vichangie ukuaji wa uchumi na
ustawi wa wananchi.
..........
Makamu wa Rais aliyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi
wa mradi wa kuendeleza utalii kanda ya kusini mwa Tanzania uliofanyika Kihesa
Kilolo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais alisema Serikali imeendelea kuandaa na
kutekeleza mipango mikakati mabali mbali kwa lengo la kuhakikisha shughuli za
utalii zinasambaa nchi nzima .
Makamu wa Rais amasema
katika kuendeleza utalii kanda ya kusini, ambapo Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imepokea mkopo mwenye masharti nafuu Dola za kimarekani
milioni 150 kutoka benki ya Dunia ambapo mradi huo utatekelezwa kwa miaka 6
kuanzia 2017/2018.
Mradi huo wenye lengo kuu la kukuza utalii na kipato kwa
wananchi kwa kuboresha miundo mbinu, kujenga uwezo katika usimamizi wa
maliasili na kuwawezesha wananchi wanaozunguka hifadhi kuzalisha kwa tija
“Kama nilivyosema
hapo awali mradi huu utajulikana kama
Resilient Natural Resource for Tourism and Growth (REGROW)
na utaanza kutekelezwa katika maeneo ya hifadhi ya Taifa za Ruaha,
Mikumi, Udzungwa na Pori la Akiba Selous “
Makamu wa Rais ameiagiza Baraza la Mazingira lililokuwa
chini ya Ofisi yake kuharakisha tathmini ya mazingira ya bonde la mto ruaha
mkuu ili kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa kwa ufanisi bila athari zozote
baadaye za mazingira.
Makamu wa Rais alielekeza taasisi zote zinazohusika zikiwemo Sekretarieti za mikoa, Halmashauri
za Wilaya na Vijiji kutoa ushirikiano wa kutosha wa kufanikisha utekelezaji wa shughuli za mradi.
“Tuhakikishe sheria
zinafuatwa na hakuna uvamizi wala shughuli za binadamu kwenye vyanzo vya maji
na hifadhi. Wahenga wanasema tunza mazingira yako yakutunze”.
Makamu wa Rais aliwashukuru benki ya Dunia kwa kukubali
kukopesha mkopo wenye masharti nafuu .
Aidha kabla ya Makamu wa Rais kuzungumza, Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla alisema Sekta ya Utalii ni
moja ya sekta za kipaumbele katika uchumi wa Tanzania ambapo takribani asilia
20 ya pato la Taifa linatokana na utalii na robo ya fedha za kigeni zinatokana
na Utalii.
0 Comments