Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Ndg. Nenelwa
Wankanga akifungua semina ya Jinsi ya kukabiliana na Vihashiria hatarishi ndani
ya Ofisi ya Bunge kwa Wakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi, Wakuu wa Vitengo na
baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Bunge iliyoanza leo katika kumbi za Bunge Mjini
Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakifuatilia semina
iliyotolewa na Wahadhiri waandimizi kutoka Chuo kikuu cha Mzumbe Jinsi ya
kukabiliana na Vihashiria hatarishi ndani ya Ofisi ya Bunge, iliyofanyika leo
katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.
Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo kikuu Mzumbe,
Ndg. Alloyce Maziku akizungumza na Wakurugenzi, Wakurugenzi wasaidizi, Wakuu wa
Vitengo na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakati akitoa maada katika
semina ya Jinsi gani ya kukabiliana na Vihashiria hatarishi ndani ya Ofisi ya
Bunge iliyofanyika leo katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Bunge wakifuatilia semina
iliyotolewa na Wahadhiri waandimizi kutoka Chuo kikuu cha Mzumbe Jinsi ya
kukabiliana na Vihashiria hatarishi ndani ya Ofisi ya Bunge, iliyofanyika leo
katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.
PICHA
NA OFISI YA BUNGE
0 Comments