Random Posts

Matukio katika Picha Ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Wilayani Sengerema

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Sengerema baada ya  kuweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kusaga nafaka na kukoboa mpunga cha Dotto Posho Mill kilichopo eneo la Bukara, Sengerema Februari 15, 2018.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Buchosa wakati alipoingia kwenye uwanja wa michezo wa Nyehunge wilayani Sengerema kuhutubia mkutano wa hadhara Februari 15, 2018.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda kidogo  cha Dotto Posho Mill, Bw.  Alexander Dotto  (kushoto) kuhusu  unga na Mchele unaozalishwa na kiwanda hicho kilichopo eneo la Bukara, Sengerema Februari 15, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Miongella.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Post a Comment

0 Comments