Kampuni
ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imezindua shindano la
Zawadi ya Chini ya Kizibo (UTC) la “Pindua Ushinde” litakalofanyika kwa
muda wa siku 45, linalotarajiwa kuisha Machi 10 mwaka huu.
Akizungumza
na wanahabari katika uzinduzi wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Masoko
MeTL, Fatema Dewji ameeleza namna ya kushiriki shidano hilo, kwamba ili
ujishindie zawadi, inatakiwa kununua maji ya Mo Maisha na Masafi yenye
ujazo kuanzia Mili lita 600 hadi lita 1.7.
“Kwa
mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tunawaletea shindano la
zawadi ya chini ya kizibo kwa bidhaa za maji. Hii ni kwa maji ya Mo
Maisha na Masafi yenye ujazo kuanzia Mili Lita 600, lita 1 na lita 1.7
ambazo huja kwako katika chupa za plastiki. hii haijawahi kutokea popote
nchini Tanzania,” amesema.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL),
Fatema Dewji akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa shindano la Zawadi
ya Chini ya Kizibo (UTC) la “Pindua Ushinde”
Amesema,
Pindua Ushinde inakupa fursa ya kujishindia zawadi ya Maji ya bure au
pesa taslimu kuanzia Sh. 1,000 hadi 100,000, ambapo ili kujionea
ulichoshinda, unatakiwa kupindua kizibo cha chupa ya maji ya Mo Maisha
au Masafi.
“Maji
ya Mo Maisha na Masafi ni safi na salama kwa afya yako na hutayarishwa
katika mazingira bora ya usafi wa hali ya juu. Pia,chupa zetu ni safi na
salama zilizorafiki kwa matumizi yako zimetengenezwa ili kukidhi
viwango vya kimataifa. Kumbuka unapokunywa maji yetu unajiepusha na
magonjwa yanayoenezwa kwa maji yasiyo safi na salama,” amesema.
Vile
vile, Fatema Dewji amezindua Kampeni ya kutunza mazingira inayofahamika
kwa jina la “Tanzania Safi” iliyolenga kuhakikisha ardhi haiharibiwi
kwa uchafu wa chupa za plastiki.
“Tutatoa
ushirikiano kuondoa chupa za plastiki zitakazoonekana mitaani ili
zitumike kama malighafi katika uzalishaji viwandani. Hii si mara ya
kwanza kufanya kampeni za utunzaji mazingira, awali MeTL ilifanya
kampeni ya utunzaji mazingira kwa kusafisha ufukwe wa Coco Beach," amesema na kuongeza.
“Pia
tuliendesha kampeni ya kuelimisha jamii namna ya kuepuka magonjwa
yanayosababishwa na matumizi ya maji yasiyo safi na salama ambapo
wataalamu wa afya walielimisha jamii.”
Naye
Meneja Mauzo wa Kiwanda cha A 1 kilicho chini ya MeTL kinachozalisha
Maji ya Mo Maisha na Masafi, Godfrey Mangungulu amesema washindi wa maji
bure na fedha kuanzia 1,000 hadi 50,000 watapewa zawadi zao waliponunua
maji, na watakaoshinda zaidi ya fedha hizo watachukua bidhaa zao kwenye
Kiwanda cha A1 kilichopo Kurasini.
“Tumeamua kurudisha fadhila kwa
jamii, kwa zaidi ya miaka 20 tunauza bidhaa zetu , hivyo tumeamua
kurudisha sehemu ya mauzo ya bidhaa zetu kwa jamii. MeTL tuajivunia
bidhaa bora na usambazaji wetu unafika nchi nzima,” amesema.



0 Comments