Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza wakati wa
mkutano kati yake na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (hayupo pichani), kuhusu namna ya kuboresha
ushirikiano katika kukuza biashara kati ya Tanzania na benki yake, uliofanyika
katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Afrika Bw. Peter Matlare akielezea umuhimu wa kushirikiana katika kukuza biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Benki yake wakati wa mkutano kati yake na Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani)
uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mjini Dodoma.
Ujumbe
kutoka Benki ya Barclays uliongozwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Barclays Afrika, Bw. Peter Matlare (kulia), wakichukua kumbukumbu wakati
wa mkutano kati yao na Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa
Wizara hiyo mijini Dodoma.
Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha
na Mipango ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip
Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakifuatilia mazungumzo kati yao na ugeni
kutoka Benki ya Barklays nchini Afrika Kusini (hawako pichani), mkutano
uliofanyika mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tano
kulia),
Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays
Afrika Bw. Peter Matlare (wa sita kushoto) wakiwa katika picha yapamoja na
baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Benki ya Barclays baada ya
kumalizika kwa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya
Fedha na Mipango Mjini Dodoma.
Benny
Mwaipaja, Dodoma
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amekutana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Barclays Kanda ya Afrika, Bw. Peter Matlare na kuiomba Benki hiyo
kuangalia uwezekano wa kutoa mkopo nafuu wa ujenzi wa miradi mikubwa inayotekelezwa
na Serikali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa viwango vya kimataifa (SGR)
mradi wa miundombinu ya umeme wa Stieglar's Gorge ili kurahakisha maendeleo ya
kiuchumi kupitia viwanda.
Amemweleza
kiongozi huyo kwamba Serikali imeimarisha uchumi Mkuu kwa kudhibiti mfumuko wa
bei ambao uko katika kiwango chatarakimu moja cha wastani wa asilimi 5.3 katika
kipindi cha miezi 6 iliyopita.
"Tumewekeza
kwenye miundombinu kama vile Elimu, maji, kilimo, afya, madini, na biashara na kwamba
katika kipindi kifupi cha miaka 2 zaidi ya viwanda 80 vimejengwa katika eneo la
Mkuranga mkoani Pwani, kutokana na fursa za uwepo wa bomba la gesi na eneo hilo
kuwa karibu na Bandari ya Dar es Salaam.
Dkt.
Mpango ameelezea pia mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) ambao
amesema utarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika nchi
zinazopakana na Tanzania hivyo kukuza biashara kwa kiwango kikubwa.
Akizungumzia
kuhusu ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme katika Bonde la mto Rufiji (Stiegler's
Gorge), Dkt. Mpango amesema lengo la mradi huo utakao zalisha megawati 2,100 za
umeme utakao kuwa wa uhakika na bei nafuu ili kukuza viwanda.
Alisema
kuwa mwelekeo wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kila biadhaa
zinazozalishwa nchini pamoja na madini, vinaongezwa thamani hapa hapa nchini
badala ya kuuzwa kama malighafi na kwamba nishati ya umeme ndiyo nguzo kuu ya
kufikia malengo hayo.
"Ili
tuweze kufikia azma hiyo tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika na wa bei nafuu
ili viwanda vyetu viweze kuzalisha kwa wingi ndio maana tunaiomba Benki yako
iweze kufikiria namna ya kushiriki katika ujenzi wa miradi hii"
Alisisitiza Dkt. Mpango.
Dkt.
Mpango ameipongeza Benki ya Barclays ambayo pia ni mwanahisa katika Benki ya
NBC kwa ahadi yake ya kutaka kuwekeza kiteknolojia katika sekta ya benki nchini
hatua ambayo itasaidia kukuza mitaji na mikopo kwa kundi kubwa la watanzania
wakiwemo wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa.
Alielezea
msimamo wake kwamba katika kukuza uchumi, Serikali inathamini mchango mkubwa wa
Sekta Binafsi na imeendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba hivi
karibuni alikuta na wadau wa Sekta ya Benki ili kusikiliza changamoto zao na
pia kuwaeleza mambo muhimu ambayo ingependa sekta Binafsi ifanye ili kufikia
malengo yanayokusudiwa.
Awali,
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Barclays anaye hudumia kundi la benki za
Barclays Barani Afrika na kwingineko Marekani na Ulaya, Bw. Peter Matlare,
ameipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia kikamilifu
uchumi wa nchi unaokua kwa wastani wa asilimia 7.
Alisema
hatua hiyo ni ya kupigiwa mfano katika nchi za Kiafrika na Duniani kwa ujumla
ambapo amesema Tanzania imekuwa ikifanya vyema katika kukuza uchumi jumuishi
unaowafikia watu wengi zaidi wakiwemo waishio mijini na vijijini.
Bw.
Peter Matlare amemhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,
kwamba Benki yake itayafanyia kazi mapendekezo ya kutaka ushiriki wake katika
ujenzi wa miradi mikubwa iliyoainishwa na Serikali kuwa kipaumbele chake.





0 Comments