Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA),Hosea Gonza Mbilinyi.
waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi wa
serikali ya mapinduzi zanzibar, hamad rashid muhamed(mwenye suti nyeupe)
kushoto kwake ni waziri wa mifugo na uvuvi, luhaga joelson mpina (mwenye
koti jekundu) na kulia kwake ni katibu mkuu uvuvi tanzania bara dkt. yohana
budeba wakiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi na watendaji wa sekta
ya uvuvi mara baada ya waziri mpina na watendaji wake kuwasili leo unguja kwa
ziara ya kikazi.
Kiongozi wa Kampuni ya Linghang kutoka china inayoshughulika
na uendelezaji wa Utalii wa Zanzibar nchini china Tom Zhang
(katikati) akiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji
wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi.
Picha
na John Mapepele
Na
John Mapepele
Serikali
imezipiga faini ya bilioni kumi na tisa meli 19 ikiwa ni shilingi bilioni
moja kwa kila meli na kuamuliwa kulipa faini hiyo ndani ya wiki mbili kwa
kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa
Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa
kutoripoti katika bandari Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara ama Tanga kwa ajili
ya ukaguzi kabla ya kutoka katika bahari kuu ya Tanzania.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, katika Ofisi za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu
zilizopo Fumba kisiwani Unguja, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina
amesema pamoja na meli hizo kuamriwa kulipa faini ya Shillingi Billioni
moja (Tshs.
1,000,000,000) kila moja zinatakiwa kurejea katika bandari
za Tanzania kwa ajili ya ukaguzi kwa kuwa leseni zao bado hazijaisha muda wake
hadi sasa ili kubaini thamani halisi ya kiasi cha fedha zitakazotozwa kwa ajili
ya samaki waliovuliwa bila kukusudia(Bycatch).
Aidha
Mpina amesema meli hizi zimetakiwa kuilipa Tanzania kiwango cha pesa kwa
mujibu wa soko la kimataifa kutokana na kuondoka na Bycatch waliyoripoti kuwa
wanayo kabla ya kutoroka.
Waziri
Mpina amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba kuiamru Mamlaka ya
uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) iwaandikie notisi wahusika wa meli hizi kuwajulisha
kuhusiana na maamuzi haya pia kuwajulisha Kamisheni ya Jodari kwenye Bahari ya
Hindi, (IOTC) kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na Tanzania dhidi ya meli hizo
ili isaidie kuwabaini na kuwachukulia sheria kwa mujibu wa Sheria husika.
Aidha
imeamriwa kwamba Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pia iandae barua/ andiko kwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili aweze kuiandikia Barua Wizara ya
Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasiliana na Flag States (Mataifa ambayo meli hizi
zimesajiliwa) ili kuwajulisha makosa yaliyotendwa na meli husika pamoja na
hatua ambazo Tanzania imechukua.
Amesema meli zote zilizotoroka zimesajiliwa
nchini China.
Wakati
huo huo Waziri Mpina amesema meli ya Tai Hong 1 imekiuka Kifungu cha 18
cha Sheria ya uvuvi wa Bahari kuu No. 1 ya Mwaka 1998 na marekebisho yake ya
mwaka 2007 pamoja na Kanuni ya 66 ya kanuni za uvuvi wa Bahari kuu za Mwaka
2009 na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kukutwa na mapezi ya papa
yasiyoendana na miili iliyokutwa kwenye meli hiyo baada ya kukaguliwa katika
bandari ya Dar es Salaam mnamo tarehe 25/01/2018-27/01/2018.
Pia
meli hii imebainika kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya
kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka
2016 kwa kuhaulisha mabaharia kutoka kwenye meli nyingine ambao idadi yao
ilikuwa mabaharia 10.
Aidha
meli hii pamoja na kukutwa na makosa hayo iliondoka nchini bila kufuata
taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa vifungu tajwa hapo juu.
Kutokana
na makosa hayo imeamriwa na Mamlaka ya Bahari kuu (DEEP SEA FISHING AUTHORITY)
kulipa jumla ya faini ya Shillingi Billion moja (Tshs. 1,000,000,000) ambapo
Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu itawasilisha notisi ya adhabu hii kwa wahusika
wa Meli hii ya TAI HONG 1.
Mbali
na Tai Hong 1 Mpina amezitaja Meli hizo zilizopigwa faini ya Bilioni moja kila
moja kuwa ni pamoja na TAI HONG NO2 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/453, TAI HONG 8 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/454, ,TAI
XIANG 2 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/455, TAI XIANG 5 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/456, TAI XIANG 1 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/457, TAI XIANG 8 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/458 na TAI
XIANG 9 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/459.
Meli
nyingine ni TAI XIANG 10 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/460, TAI XIANG
7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/461, TAI XIANG 6 yenye namba ya
leseni TZ/DSFA/EEZ/462, TAI HONG 6 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/463, TAI HONG 7 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/464,
XIN SHIJI 81 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/466, XIN SHIJI 82 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/467, XIN SHIJI 83 yenye namba ya leseni
TZ/DSFA/EEZ/468, XIN SHIJI 86 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/470, XIN
SHIJI 72 yenye namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/471, XIN SHIJI 76 yenye
namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/472 na JIN SHENG 1 yenye namba ya
leseni TZ/DSFA/EEZ/473.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yohana Budeba amewataka
wawekezaji kwenye bahari ya Tanzania kuwa waaminifu na kuzingatia
masharti na taratibu za kisheria ili nchi na wawekezaji waweze kunufaika.
“Taratibu
zipo wazi ni muhimu kuzinangatia sheria namna nyingine tutaendelea
kusimamia sheria za nchi yetu kwa faida ya sasa na vizazi vya baadaye”
Alisisitiza Dkt. Budeba
Amesema
hatua iliyochukuliwa na Serikali ya kuzipiga faini meli hizo ni
somo kwa meli nyingine na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa
yoyote atakayebainika kutenda makosa ya uvuvi haramu katika bahari
na maziwani.
Aidha
amesema Serikali ipo tayari kufanya biashara na mtu yoyote ambaye
atazingatia masharti ya nchi, na kwamba taifa linajipanga ili kuwa na makampuni
yake ya TAFICO na ZAFICO yatakayoshuhulika na uvuvi ili kunufaika na raslimali
za uvuvi kama ambavyo inafanyika katika nchi mbalimbali duniani.
Amesema
hatua hiyo itasaidia kukuza ajira kwa wananchi, uchumi wan chi na kuanzisha
viwanda vya kuchakata samaki na mazao yake.
Aliwashukuru
wadau wote wanaoshiriki kwenye mapambano ya uvuvi ambapo kipekee
alilishukuru shirika lisilo la kiselikali la Sea worrior kwa kutoa mchango
mkubwa kwenye operesheni Jodari ambayo imefanywa na wadau mbalimbali
nchini.




0 Comments