Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako walioshiriki kikao kazi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani). Watumishi walipata fursa ya kuuliza masuala mbalimbali ya kiutendaji na kupewa ufafanuzi.
Mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako akitumia fursa ya kuwasilisha hoja kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi mjini Makambako.
Serikali kuwapangia baadhi
ya walimu wa shule za sekondari kufundisha katika shule za msingi ni moja ya
hatua katika kuongeza ufanisi na kuleta mgawanyo sawa wa walimu katika shule za
sekondari na msingi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema hatua hiyo
haimaanishi kuwa walimu wanaotoka katika shule ya sekondari kwenda kufundisha
msingi wameshushwa cheo.
Dkt. Ndumbaro ametoa
ufafanuzi huo katika kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mji wa
Makambako. Amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuondoa upungufu wa walimu
katika shule za msingi na kuimarisha utoaji wa elimu.
Dkt. Ndumbaro ameainisha kuwa sifa za kufundisha na kiwango cha elimu
zinaendana na mabadiliko yanayotokea duniani, hivyo mwalimu mwenye elimu ya
kiwango cha Shahada ya kwanza kufundisha shule ya msingi isionekane ni jambo la
ajabu.
Katibu Mkuu Dkt. Ndumbaro amewaambia watumishi wa umma maendeleo katika
sekta yoyote, ikiwamo ya elimu yanakuja na mabadiliko hivyo wapokee mabadiliko
na kufanya kazi ili kufikia lengo.
Florence Lawrence
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano
OFISI
YA RAIS (UTUMISHI)
20 Februari, 2018.
0 Comments