Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye (aliyesimama) akiwatunuku vyeti wahitimu 529 (hawapo pichani)
wa astashahada na stashahada wa Chuo cha Bandari Dar es Salaam kwenye mahafali
ya 16 ya Chuo hicho yaliyofanyika Chuoni hapo jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Bodi ya
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania mzee Renatus Mkinga akimwakilisha Mwenyekiti
wa Bodi ya Bandari ya Dar es Salaam Prof. Ignas Rubalatuka, akiwaasa wahitimu
(hawapo pichani) wa chuo hicho wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho
yaliyofanyika chuoni hapo
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye akizungumza na wahitimu, wanachuo, wafanyakazi, wageni
waalikwa na wazazi (hawapo pichani) kwenye mahafali ya 16 ya Chuo cha Bandari
Dar es Salaam yalyofanyika chuoni hapo Dar es Salaam
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akimtunuku cheti kwa kufaulu vizuri masomo
yake mmoja wa wahitimu Bi. Shekha Habibu Humudi wakati wa mahafali ya 16 ya
Chuo cha Bandari Dar es Salaam yaliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Joseph Kakeneno na wa
kwanza kushoto ni mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
mzee Renatus Mkinga
Mgeni rasmi wa
Mahafali ya 16 ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta
Nditiye (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu
wa Chuo hicho. Aliyeketi wa kwanza kushoto ni mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania mzee Renatus Mkinga na wa kwanza kulia ni Mkuu wa
Chuo hicho Dkt. Joseph Kakeneno
Mmoja wa wajumbe wa
Bodi ya Chuo cha Bandari Dar es Salaam Bi. Nuru Mhando (wa kwanza kulia)
akimkaribisha mgeni rasmi wa Mahafali ya 16 ya Chuo hicho Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto)
alipowasili chuoni hapo. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt.
Joseph Kakeneno
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) pamoja na uongozi wa Menejimenti wa Mamlaka hiyo kutoa nafasi
kwa wanachuo wa Chuo cha Bandari Dar es Salaam kufanya mafunzo kwa vitendo
wakati wa masomo yao kwenye bandari zote nchini.
Mhandisi Nditiye
ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 16 ya Chuo cha Bandari Bar
es Salaam ambapo jumla ya wahitimu 521 wametunikiwa cheti cha kuhitimu mafunzo
yao katika ngazi ya elimu ya astashahada na stashahada ya mafunzo ya aina
mbalimbali ikiwemo mafunzo ya usimamizi wa shughuli za meli na bandari;
uhandisi na usimamizi wa matengenezo; zimamoto na usalama; masoko na
mawasiliano ya umma; usimamizi wa wakala wa forodha na usafirishaji wa mizigo;
usimamizi wa mipango ya uchukuzi na usafirishaji; na utawala na biashara.
Ameongeza kuwa nia ya
Serikali ni kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ya kuboresha bandari zetu, kuongeza ufanisi na tija katika
utendaji kazi wa sekta ya usafirishaji majini ili kukuza uchumi na kuongeza
mapato la taifa letu.
Pia, wakati akisoma
hotuba yake kwa wahitimu hao, Mhandisi Nditiye amewataka wahitimu hao kutumia
vyeti vyao na taaluma waliyoipata vizuri kwa kukitangaza vema Chuo cha Bandari
Dar es Salaam aidha kwa kujiajiri au kuajiriwa ndani na nje ya nchi.
Aidha,
amesisitiza kuwa wanaoajiriwa kuwa wafanyakazi wa bandari mbalimbali wawe
wamehitimu chuo na kuwa na elimu inayotakiwa. Vile vile amemuagiza Mkuu wa Chuo
cha Bandari Dkt. Joseph R. Kakeneno kujenga zahanati kwa ajili ya kutoa huduma
za tiba kwa wanachuo na jamii ya Chuo hicho.
Naye mjumbe wa Bodi ya
Mamlaka ya Usimamzi wa Bandari Tanzania mzee Renatus Mkinga ambaye amemwakilisha
Mwenyekiti wa bodi wa Mamlaka hiyo Prof. Ignas Rubalatuka, katika mahafali hayo
amewataka wanachuo kusoma kwa bidii ili waweze kuajiriwa na kufanya kazi mahali
popote iwe ndani au nje ya nchi.
Aidha, wahitimu wa
chuo hicho wamemshukuru Dkt. Kakeneno kwa kufanikisha upatikanaji wa ithibati sita
za kozi mbalimbali kati ya ithibati nane zinazohitajika. Hivyo, wamemuomba
mgeni rasmi Mhandisi Nditiye kumsaidia Dkt. Kakeneno kupata ithibati nyingine
mbili zilizosalia.
Katika hatua nyingine,
Mhandisi Nditiye ametoa mwezi mmoja kwa Chuo cha Bandari Dar es Salaam kwa
kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
kurudisha majengo ya Chuo hicho, uwanja wa michezo na mali zote zilizokuwa
zinatumiwa na Chuo cha Hoteli na Utalii ambazo ziko ndani ya eneo la Chuo cha Bandari ya Dar es Salaam
yarudishwe kwenye Chuo cha Bandari.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 Comments