Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa
wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na
wadau wengine wa usalama na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwa ni
pamoja na kukamata watuhumiwa watatu wa matukio mawili tofauti katika
Wilaya ya Mbeya na Chunya.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA MBALIMBALI.
Mnamo tarehe 02 Februari, 2018 majira ya saa 20:00 usiku huko
katika Kitongoji cha Kasanga – Kanyika, Kijiji cha Lupa – Market, Kata
ya Kasanga, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata majambazi wawili ambao
wamefahamika kwa majina ya 1. FITINA RUBEN mwanamume [30] na 2. SUMBUKO
SANGA mwanamume [32] wote wakazi wa Chunya mjini.
Baada ya kukamatwa na kufanyiwa
upekuzi, watuhumiwa hao wa tukio la ujambazi walikutwa na silaha na vitu
mbalimbali ambavyo huvitumia katika uhalifu. Silaha/Vitu hivyo ni:-
- Bunduki moja aina ya short gun iliyotengenezwa kienyeji.
- Risasi moja inayotumiwa na silaha aina ya short gun.
- Manati moja.
- Maski Tatu
- Rungu moja
- Panga moja
- Nondo moja
- Banio moja (praise)
- Koti moja la kijeshi.
- Gloves moja.
- Mzula mmoja na
- Simu moja aina ya Tecno ambayo mmiliki wake bado hajafahamika.
Awali mnamo tarehe 31 Januari,2018
majira ya saa 15:00 Alasiri huko katika Kitongoji cha Kasanga –
Kanyika, Kijiji cha Lupa – Market, Kata ya Kasanga, Tarafa ya Kiwanja,
Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Mfanyabiashara wa Madini anayefahamika
kwa jina la MWILE SINJALE mwanamume [40] Mkazi wa Kasanga – Kanyika
aliuawa kwa kupigwa risasi moja kichwani kwa kutumia silaha/bunduki aina
ya Shot gun na watu wanne wanaume ambao waliokuwa na bunduki hiyo na
mapanga 3 huku nyuso zao wakizifunika kwa mask ambao baada ya tukio hilo
watu hao walifanikiwa kutokomea porini/msituni.
Aidha marehemu alikuwa
akitokea Chunya mjini kwa kutumia usafiri wa pikipiki yake akiwa
amepakiwa na mfanyakazi wake na alikuwa amebeba mikate mikubwa miwili
kwenye Lasket ya mgongoni, hivyo watu hao walidhani amebeba pesa na
kisha kumvamia na kumuua.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi
la Polisi lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata majambazi
wawili kati ya wanne ambao inadaiwa kuhusika katika tukio hilo la tarehe
31 Januari, 2018. Baada ya mahojiano, watuhumiwa wamekiri kuhusika na
mauaji ya mfanyabiashara huyo wa madini. Upelelezi unaendelea ikiwa ni
pamoja na kuwasaka watuhumiwa wengine wawili waliohusika katika tukio
hilo la mauaji ya Mfanyabiashara huyo.
KUPATIKANA KWA MTUHUMIWA WA WIZI WA MTOTO.
Mnamo tarehe 03 Februari, 2018
majira ya saa 12:00 Mchana huko maeneo ya mtaa wa Mponja – Uyole, Kata
ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Viongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
walifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la HAPPY
CHARLES [24] Mama Lishe, Mkazi wa Airport ya Zamani akiwa na mtoto
mchanga jinsia ya kike aliyemuiba Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Awali mnamo tarehe 01
Februari, 2018 majira ya saa 04:00 usiku huko katika wodi ya watoto
Hospitali ya Mkoa wa Mbeya iliyopo Kata ya Forest Mpya, Tarafa ya
Iyunga, Jijini Mbeya, mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la SARAH
MWASANGA [35] Mkazi wa Iganzo akiwa katika wodi ya wazazi Hospitalini
hapo baada ya kujifungua mtoto wa kike aligundua kuibiwa kwa mtoto huyo
na mtu asiyefahamika.
Kutokana na tukio hilo,
uongozi wa Hospitali hiyo ulitoa taarifa kituo kikuu cha Polisi
[Central] na ndipo upelelezi kuhusiana na tukio hilo ulianza kufanyika.
Taarifa za siri zilipatikana na kubainisha kuwa huko maeneo ya Airport
ya zamani kuna mama mmoja aitwaye HAPPY CHARLES [24] Mkazi wa Airport
ambaye hapo awali alikuwa akimdanganya mume wake aitwaye CHILUBA PETER,
Dereva Taxi Hospitali ya Rufaa Mbeya na Mkazi wa Airport kuwa ni
mjamzito na kwamba amejifungua mtoto wa kike tarehe 31 Februari, 2018 na
ndipo ufuatiliaji wa kuwapata watu hao ulianza.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa
maeneo ya mtaa wa mponja – uyole, kata ya igawilo, tarafa ya iyunga kwa
mama yake mzazi aitwaye MARY AKIMU [59] Mkazi wa Mtaa wa Mponja – Uyole
ambapo alikwenda kwa ajili ya kupata huduma za uzazi. Upelelezi
unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani
kujibu tuhuma zinazomkabili.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa jamii
kuondokana na tamaa ya kutaka utajiri kwa njia zisizo halali kwa
kujihusisha na uhalifu na badala yake watafute shughuli halali kwa ajili
ya kujipatia kipato. Aidha anatoa onyo kali kwa yeyote atakayejihusisha
na uhalifu kuwa Jeshi la Polisi halitakuwa na huruma na kuhakikisha
anakamatwa na kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.
Pia Kamanda MPINGA
anatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika
kuzuia uhalifu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za mtu/watu au kikundi
cha watu wanachokitilia mashaka ili upelelezi ufanyike dhidi yao.
Imesainiwa na:
[MOHAMMED R. MPINGA – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

ambapo alikwenda kwa ajili ya kupata huduma za uzazi.
Upelelezi
unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani
kujibu tuhuma zinazomkabili.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa jamii
kuondokana na tamaa ya kutaka utajiri kwa njia zisizo halali kwa
kujihusisha na uhalifu na badala yake watafute shughuli halali kwa ajili
ya kujipatia kipato.
Aidha anatoa onyo kali kwa yeyote atakayejihusisha
na uhalifu kuwa Jeshi la Polisi halitakuwa na huruma na kuhakikisha
anakamatwa na kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria.
Pia Kamanda MPINGA
anatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika
kuzuia uhalifu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za mtu/watu au kikundi
cha watu wanachokitilia mashaka ili upelelezi ufanyike dhidi yao.
Imesainiwa na:
[MOHAMMED R. MPINGA – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:
Post a Comment