Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge
ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba akizungumza na Wajumbe wa
kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Mkoa wa Simiyu (hawapo kwenye
picha) walioongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kupokea
na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018
pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kulia
ni katibu kamati wa kamati hiyo, Ndg. Victor Leonard
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala
na Serikali za Mitaa, Mhe. Saada Mkuya akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo
pamoja na viongozi wakuu kutoka Mkoa wa Simiyu (hawapo kwenye picha) walioongozwa
na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kupokea na kujadili Taarifa
kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya
Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 katika kikao kilichofanyika leo
ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe wa kamati, Mhe. Lucia
Mlowe
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za
Mitaa wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya
Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa
Fedha 2018/2019. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhe. Jumanne Sagini
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge
ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia mazungumzo wakati wa kupokea na
kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018
pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kutoka
kushoto ni Mhe. Lucia Mlowe, Mhe. Saada Mkuya, Mhe. Mwantum Haji na Mhe. George
Lubeleje
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
0 Comments