Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya
Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania
(SHIMMUTA) uliofanyika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Machi 27, 2018 mjini
Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Mashirika ya Umma
na Makampuni Binafsi kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki michezo katika maeneo yao
ya kazi lakini pia wawaruhusu wafanyakazi hao kushiriki Michezo ya SHIMMUTA.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya
Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amesema michezo ni muhimu
sana kwenye Tanzania ya Viwanda kwani michezo husaidia mwili kuwa wenye afya
bora na utendaji wao wa kazi unakuwa mzuri zaidi.
Makamu wa Rais amesema yeye alikuwa
mwanamichezo mzuri wa mpira wa pete (netball) lakini kwa sasa anafanya mazoezi
kidogo kidogo asubuhi na jioni.
“Najua
Umuhimu wa kufanya mazoezi kwa sababu nikiacha kufanya mazoezi nadorora na
katika nafasi hii ukidorora unadorora mpaka akili na kazi zitakushinda”
Makamu wa Rais aliwasihi Viongozi wa Michezo
kusimamia masuala ya michezo katika maeneo ya kazi na kuwataka Viongozi wa
Taasisi kuweka bajeti ya michezo kwa ajili ya kushiriki michezo ya SHIMMUTA.
Makamu wa Rais amesema ilani ya uchaguzi ya
Chama Cha Mapinduzi ya 2015- 2020 imeleekeza kuendeleza michezo sehemu za kazi.
Aidha Mwenyekiti wa SHIMMUTA Ndugu Hamis
Mkanachi alimpongeza Makamu wa Rais kwa juhudi anazozifanya katika kukuza
michezo nchini.


0 Comments