Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Mhe.
Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi pamoja na Balozi wa Tanzania nchini
Rwanda Mhe.
Ernest Mangu ambao walifika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la
kumuaga kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Mhe.Ernest Mangu na Meja Jenerali Mstaafu
Simon Marco Mumwi wa Urusi leo wamekutana na kuzungumza na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mjini
Dodoma.
Mabalozi hao walifika kwenye makazi ya Makamu wa Rais,
Kilimani Dodoma kwa lengo la kumuaga ,walimuahidi
Makamu wa Rais kufanya kazi kwa ajili ya Tanzania.
Wamemuambia Makamu wa Rais wanajua dhamana kubwa
waliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli na dhamira yake ya Tanzania ya Viwanda .


0 Comments