Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya
pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia
Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati
kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
Na Hamza Temba - WMU-Dodoma
.............................. ............
Kufuatia
jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kutafuta wawekezaji wa
Kimataifa kwa ajili ya kuwekeza katika sekta utalii hapa nchini, Kampuni
ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China
imejitokeza kwa lengo la kuwekeza katika utoaji wa huduma za kitalii
zenye ladha na mandhari ya Kichina.
Mwenyekiti
wa Kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Tony, amesema
kampuni hiyo imepanga kujenga hoteli za kitalii za kichina katika mji wa
Karatu jijini Arusha na Serengeti mkoani Mara.
Akizungumza
na Waziri wa Maliasil na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ofisini kwake
mjini hapa jana kwa ajili ya kutambulisha mradi huo, Tony alisema mradi
huo ni mahsusi kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii wa China
wanaotembelea Tanzania.
Alisema
kupitia mradi huo jumla ya magari 500 ya safari za utalii yatanunuliwa
(Safari Cars) kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii hao wakati wa
kutembelea maeneo ya vivutio hapa nchini.
Pamoja
na magari hayo alisema kampuni hiyo pia imepanga kuanzisha safari za
moja kwa moja za ndege kutoka China hadi Tanzania ili kupunguza muda wa
usafiri na gharama.
"Kupitia
mradi huu, tunategemea kuhudumia watalii 200,000 kwa mwaka kutoka
nchini China na kutengeneza ajira zaidi ya 200 kwa Watanzania" alisema
Tony.
Alisema
kwa sasa ni watalii 35,000 tu kutoka China wanaotembelea Tanzania kwa
mwaka, na kwamba kupitia mradi huo idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.
Naye
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema mradi huo
umekuja wakati muafaka wakati huu Serikali kupitia Wizara yake
imeshaweka mikakati mahususi ya kupanua wigo wa soko la utalii nchini
China.
Alisema
miongoni mwa mikakati hiyo inayolenga kuvutia watalii zaidi ya 200,000
kwa mwaka katika kipindi cha muda mfupi wa miaka mitatu, ni
kuwakaribisha wachina wenyewe kuja kuwekeza kwenye mahoteli na huduma
zenye ladha na mandhari ya kikwao. Mataifa mengine ni Israel, Urusi na
Oman.
Alisema kwa sasa ni idadi ndogo tu ya watalii wa China wanaotembelea Tanzania ukilinganisha na ukubwa wa soko la nchi hiyo.
Aliahidi
kuwapa ushirikiano wawekezaji hao ikiwa ni pamoja na kuwapa maeneo kwa
ajili ujenzi wa hoteli hizo za kitalii ndani ya maeneo ya hifadhi ili
kuwezesha ongezeko la watalii kutoka nchini humo.
"Kwa
yale maeneo mtakayohitaji ambayo yapo nje na maeneo yetu ya hifadhi
tunayoyasimamia, tutawasiliana na mamlaka husika ili muweze kuapatiwa
maeneo ya kuanzisha uwekezaji huo muhimu kwa taifa" alisema Dk.
Kigwangalla.
Aliwataka
pia wawekezaji hao kupitia taratibu zote za kuwekeza hapa nchini ikiwa
ni pamoja na kujisajili katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
Kusajili kampuni ya utalii hapa nchini na kuwasilisha andiko la mradi na
namna ya utekelezaji wake.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na
wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing
kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo
ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
Wawekezaji
wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini
China wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Kigwangalla ofisini kwake mjini
Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi flash yenye
picha za wanyamapori wa Tanzania Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya
Tibet Dexin Financia Leasing, aliyefahamika kwa jina moja la Tony kutoka
nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo
ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza hapa nchini katika ujenzi wa
mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
Waziri Kigwangalla akiendelea na mazungumzo na wakezaji hao.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na
wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing
kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo
ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
Mazungumzo yakiwa yanaendelea.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na wawekezaji
wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini
China ofisini kwake mjini Dodoma jana baada ya kampuni hiyo kuwasilisha
mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
0 Comments