Random Posts

Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Yapokea Samani

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Angeline Mabula, akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa hafla fupi ya kugawa vifaa vya Samani kwa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Angeline Mabula, akijaribu Kiti, moja ya kifaa cha Samani, alivyokabidhi kwa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya; Kulia kwake ni; Assessor Ramadhani (mwenye miwani), Mwenyekiti – Ilala; John Bigambo na Mwenyekiti  mwingine Ilala; Bi Mwenda 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Angeline Mabula, akimshika mkono Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ilala; Mhe. Chenya kuashiria Makabidhiano rasmi ya Samani kwa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya. Kulia ni; Assessor Ramadhani (mwenye miwani), Mwenyekiti – Ilala; John Bigambo na Mwenyekiti  mwingine Ilala; Bi Mwenda

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Angeline Mabula, akisisitizia kwa Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi, Nyumba na Wilaya wa Ilala na Kinondoni kuhusu Utendaji bora wa kazi na umakini wa matumizi ya Samani alizokabidhi kwa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya.


Na Kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. Angeline Mabula, amekabidhi vifaa vya Samani kwenda kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya 12 nchini.


Makabidhiano ya Samani hizo, ambapo jumla ya thamani yake ni Tsh. 112,923,404, vimenunuliwa na Mradi wa maboresho ya Sekta ya Ardhi, ambao unatekelezwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia;  Samani hizo ni pamoja na Meza, Viti, Mabenchi, Kabineti, Shelfu na Kabati za kuhifadhi majalada ya kesi, ambavyo vitaenda katika  ofisi nane za mabaraza ambazo ni Kinondoni, Moshi, Lindi, Kibaha, Dodoma, Tabora, Chato na Musoma.

Akikabidhi samani hizo jijini Dar es Salaam, Mhe. Mabula alisema Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ni miongoni mwa vyombo vilivyoundwa chini ya Kifungu cha 167 cha Sheria ya Ardhi, sura ya 113 kwa ajili ya kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusu migogoro inayotokana na matumizi ya ardhi nchini. 

Vilevile, uanzishwaji wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya unazingatia Sheria ya Mahakama za Ardhi sura ya 216 kifungu cha 22 kifungu kidogo cha kwanza (22 (1)).

Aidha, alisema Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya 53 yamekwisha kuanzishwa nchi nzima na yanafanya kazi ya kusikiliza na kuamua mashauri ya migogoro inayotokana na matumizi mbalimbali ya ardhi. Alisema;

 “Nawakumbusha watumishi wote wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutimiza majukumu yao kwa weledi na kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo na itakayokuwa inatolewa ili kuboresha utoaji wa huduma ya utatuzi wa migogoro itokanayo na matumizi ya ardhi”.

Aliendelea kusema kwamba Idadi ya migogoro inayotokana na matumizi ya ardhi imeendelea kuongezeka siku hadi siku; 

 “Napenda kuwakumbusha wananchi kutumia huduma za Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na kufuata taratibu za utatuzi wa migogoro inayotokana na matumizi ya ardhi ili kupata ufumbuzi wa migogoro hiyo kwa mujibu wa sheria”.

 Alisema., na kuwakumbusha wananchi kutumia Ofisi za Wasajili Wasidizi wa Mabaraza katika Kanda kwa ajili ya kutatua kero zao kabla ya kuwasilisha kero hizo katika ngazi ya wizara.

Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ni miongoni mwa vyombo vilivyoundwa chini ya Kifungu cha 167 cha Sheria ya Ardhi, sura ya 113 kwa ajili ya kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusu migogoro inayotokana na matumizi ya ardhi nchini. Vilevile, uanzishwaji wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya unazingatia Sheria ya Mahakama za Ardhi sura ya 216 kifungu cha 22 kifungu kidogo cha kwanza (22 (1)).

Post a Comment

0 Comments