Paparazi tayari wameshaanzisha
uvumi kama ilivyo ada, ambapo safari hii wakiihusisha kampuni kinara katika
uzalishaji wa simu za mkononi TECNO,ikitajwa zaidi midomoni mwa watu, tetesi
zaidi zinaihusisha kampuni hiyo pendwa na ujio wa toleo jipya ikiwa ni
muendelezo wa jamii ya Camon inayosemekana kuzinduliwa nchini Nigeria, siku na
saa bado havikuwekwa wazi.
Inasemekana kwamba simu
hiyo itaendana na uchumi wa Afrika ikikadiriwa kuwa na bei nafuu, hivyo nadhani
wa Afrika wanacho cha kujivunia
Swali ni kwamba je ni kweli
TECNO watakuja na toleo jipya kama inavyosemekana midomoni mwa wadau mbali
mbali, bado hakujakuwa na taarifa rasmi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika
Mara nyingi
TECNO inapohusishwa kuhusu toleo jipya bhaasi huwa kweli,je awamu hii TECNO
wanakipi cha tofauti? Maswali yamekua mengi yakiacha wadau vinywa wazi wakiwa
na shauku ya kutaka kuona ni nini TECNO watakachoingiza sokoni ikiwa ni
muendelezo wa Camon.
Kwa maelezo
zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.com/tz


0 Comments