Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akikabidhi mabati kwa ajili ya kuezeka nyumba ya Muasisi wa Chama
Cha Mapinduzi Bi. Mrashi ambayo inajengwa na wanachama wa CCM Sizini
wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha huduma ya
Mama na Mtoto Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini
Pemba.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi Bi. Mrashi nyumbani
kwake Muasisi huyo Sizini wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimia wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha huduma ya
Mama na Mtoto Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini
Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan azungumza na watoto wa kike mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya cha huduma ya
Mama na Mtoto Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni, mkoa wa Kaskazini
Pemba.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
…………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa
wa Kaskazini Pemba kushirikiana katika shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais ameyasema hayo
wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Afya cha Huduma
ya Mama na Mtoto Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini
Pemba.
Kituo hicho cha Mama na Mtoto cha
Shumba Vyamboni kitatoa huduma za Mama na Mtoto ambapo jumla ya Wananchi
5,593 wakiwemo wanawake wenye uwezo wa kuzaa 1543 na watoto chini ya
umri wa miaka mitano 984 watapata huduma bora ya uzazi, lishe na ustawi
wa mama na mtoto.
Vijiji vitakavyofaidika na huduma
ya kituo hicho ni pamoja na Kibubunzi, Kikunguni, Mihogoni, Nyuma ya
Mti, Mgeninje, Utaani, Shumba vya Mboni, Uwondwe, Mamoja, Gombe, Uwaani
na Bule.
Katika ziara hiyo yenye lengo la
kuhimiza shughuli za maendeleo Makamu wa Rais alikagua ujenzi wa Skuli
ya Sekondari ya Micheweni pamoja na kumtembelea Muasisi wa Chama Cha
Mapinduzi Bi. Mrashi ambapo alimkabidhi mabati ya kuezekea nyumba yake
inayojengwa na wanachama wa chama cha Mapinduzi katika eneo la Sizini.
Mwisho Makamu wa Rais aliweka jiwe
la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM la Ukunjwi ambapo aliwaambia wakina
Mama kuwa mstari wa mbele katika kuonesha njia ya kuwa kiongozi bora.






0 Comments