Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiweka jiwe la msingi
la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba, Machi 20,2018
(Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipeana mikono na
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuweka
jiwe la msingi
la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
(Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi
la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea mifuko ya
saruji zaidi ya elfu sita kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya
Tanga Cement Bw.
Lawrence Masha
jiwe la msingi
la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
(Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipeana mikono na
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuwasili katika
uwekaji jiwe la msingi
la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
(Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro akitoa hotuba yake.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro
kuwachukulia hatua mara moja askari polisi ambao wamekiuka maadili na taratibu
za jeshi hilo katika mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuwekwa kwa jiwe
la msingi wa ujenzi wa nyumba 36 za askari polisi katika eneo la Mfikiwe,
wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi nchini
kwa kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na yenye amani pia alitoa pongezi kwa Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni kwa kusimamia vyema zoezi la
ujengaji nyumba za Polisi.
Makamu wa Rais pia alitoa pongezi kwa kampuni ya Twiga
Cement kwa kutoa Saruji mifuko zaidi ya elfu sita pamoja na kampuni za Shubash
Patel kwa kuchangia vifaavingine vya ujenzi.
Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Mhandisi
Hamad Masauni alipongeza Jeshi la Polisi kwa kupambana na biashara haramu ya
madawa ya kulevya na kusema yeyote atakayevunja sheria achukuliwe hatua bila
kujali wadhifa au umaarufu wake.
Kwa Upende wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ameahidi
kufanya kazi kwa taratibu na sheria lakini pia alitoa wasihi kwa wanasiasa
wanaochochea vurugu kwani wao watachukuliwa kama wahalifu na si wanasiasa.
Ziara ya Makamu wa Rais imekamilika leo ambapo pia
alitembelea Hospitali ya Abdala Mzee ambapo alijionea vifaa vya kisasa
vilivyowekwa na huduma bora zinazotolewa.
Makamu wa Rais pia aliweka mawe ya Msingi katika ujenzi
wa madarasa katika skuli ya sekondari ya Ali Khamis Camp pamoja na ujenzi wa Tawi
la Chama Cha Mapinduzi Ole.










0 Comments