Mkurugenzi
wa Australia Tanzania Society, James Chialo akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za
Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi vitanda 14. Katikati ni Mkuu wa
Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona, makabidhiano hayo yamefanyika katika Hospitali hiyo Machi 20, 2018.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Dkt. Julieth Magandi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla kukabidhiwa
vitanda 14 na magodoro 12 ambayo yametolewa na Australia Tanzania Society. Kulia
ni Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo na kushoto ni Mkuu wa
Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
Mkurugenzi
wa Australia Tanzania Society, James Chialo akizungumza na waandishi wa habari
leo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo.
Muuguzi Alice Msonda na Velena Joahackim wakitandika kitanda baada ya
kukabidhiwa vitanda na magodoro na Australia Tanzania Society.
PICHA NA
JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Machi 20, 2018 imepokea msaada wa
vitanda 14, magodoro 12 pamoja na drip
stands kutoka Australia Tanzania Society ambavyo vitasaida kuimarisha utoaji wa
huduma hospitalini hapo.
Akipokea msada huo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH,
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Juliethi
Magandi amesema kwa muda mrefu hospitali imekua na ushirikiano na tasisi hiyo katika
masuala mbalimbali ikiwemo kufanya upasuaji
wa ubingwa wa juu.
“Kipekee nichukue fursa hii kuwashukuru rafiki zetu hawa
Australia Tanzania Society kwa msaada huu walioutoa kwani tumekua tukishirikiana kwa
zaidi ya miaka mitatu sasa,”. amesema
Dkt. Magandi.
Amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina jumla ya vitanda 1,507
na kwamba kina mama wajawazito na watoto pekee wanatumia karibu ya nusu ya vitanda hivyo.
“Hivyo msaada
huo umekuja wakati muafaka kwani
hospitali bado ina mahitaji kutokana na kutoa huduma zake kila siku kwa saa 24,”.
“Kati ya vitanda hivi 14 tulivyopewa , sita
tumevileta wodi 35 kwa ajili ya kina
mama na vingine 8 tumepeleka ICU namba moja na ICU namba mbili’’ amefafanua
Dkt. Magandi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo amesema msaada huo
umegharimu zaidi ya shilingi milioni 25 na kwamba lengo ni kuboresha huduma za
afya hususani katika hospitali za Umma.
“Kutoa ni
moyo si utajiri tutaendelea kushirikiana katika kuboresha huduma za afya kadiri
hali inavyoruhusu nitoe wito kwa wadau
wengine kuendelea kushirikiana ili tuboreshe huduma za afya nchini ‘’amesema
Bwana Chialo.
0 Comments