Na Tiganya Vincent
RS TABORA
KAMATI ya Bunge va Bunge ya Kudumu ya Miundombinu imeiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuanza ujenzi wa mitaro katika Uwanja wa Ndege wa Tabora ambayo itawezesha maji ya mvua kutoka kwenye eneo hilo ili kuzuia mmomonyoko wa aridhi ulianza kujitokeza na kuwa tishio ambalo linaweza kuharibu njia za kutua na kurukia ndege.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge va Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Moshi Kakoso wakati ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea Uwanja huo kujionea utekelezaji wa mradi wa ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja hicho.
Alisema ujenzi usipofanyika haraka upo uwezekano wa mvua zinazoendelea kunyesha zikasababisha uwepo wa maji mengii ambayo yatavunja njia za ndege za kutua na kuruka na hivyo kuisababishia hasara Serikali kutoka na fedha nyingi ambazo imeshaziwekeza katika mradi huo.
“Mheshimiwa Naibu Waziri tunakuomba utuitie Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ili aje atueleze kwa kina kuhusu mpango aliouandaa kuhakikisha anaokoa Uwanja huu usije ukammomonyolewa na maji kwa sababu ya kutokuwepo kwa mitaro ya kutoa maji mahali hapa” alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema ni vema wakaeleza kama Mkataba wa upanuzi na ukarabati wa uwanja huu haukuweka suala la ujenzi wa mitaro ambayo itawezesha maji kutoka uwanjani na kwenda nje.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa aliwaahidi Wajumbe wa Kamati hiyo kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha warekebisha mitaro hiyo ili uwanja usije ukaharibika kutokana na maji ya mvua ambayo yanakosa wekekeo.
Alisema katika kuhakikisha hatua zinachukuliwa haraka amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa TAA kukutana na Kamati hiyo ili waweze kumpa ushauri ambao utamwezesha kutekeleza kazi hiyo.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania Mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze alisema ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora umekamilika kwa asilimia 97 na kuongeza kilichobaki ni ujenzi wa uzio.
Alisema kazi nyingine ilibaki ni uendeshaji wa mafunzo na makabidhiano ya mfumo wa taa na mitambo ya kuongozea ndege(AGL, DVOR na DME)

0 Comments