Random Posts

Wabunge Wataka Stendi ya Tabora Ijegwe Haraka Vibanda vya Abiria


Na Tiganya Vincent
RS TABORA
17 March 2018
KAMATI ya Bunge va Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa imeiagiza Halamshauri ya Manispaa ya Tabora kuhakikisha ndani ya mwezi huu wanajenga vibanda katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendeyo mikoani kwa ajili abiria kupunzikia wakati wakisubiri usafiri.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge va Bunge ya Kudumu ya Bunge va Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa Jasson Rweikiza wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea mbalimbali ili kujionea hali ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Alisema hali iliyopo sasa sio nzuri na inawasababishia adha wasafiri na kuongeza kuwa vibanda hivyo vitasaidia kuwaondolea wasafiri adha ya kupigwa jua na kunyeshewa mvua wakati wanawasili kutoka maeneo mbalimbali au wakati wakisubiri usafiri.

“Ndugu zangu mumeona hata sisi imebidi tutafute mti ndio kufanyie kikao chetu hiki…ni lazima mjenge sehemu ya abiria kukaa na kujikinga kama wakati wa mvua au jua kali…msiwaache wasafiri waendelee kuteseka” alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ni vema Halmashauri iongeze nguvu katika ukusanyaji wa mapato kutokana na vyanzo mbalimbali vilivyopo katika Stendi hiyo.

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini aliutaka uongozi wa Tendi hiyo kuhakikisha Mawakala wa Mabasi awawabughuzi wasafiri wanaitaji kusafiri wanaingia na kutoka mkoani humo.

Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandegea aliitaka Halmashauri ya Manispaa hiyo kuhakikisha wasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato katika huduma mbalimbali ikiwemo vyoo ambapo alisema mapato ya shilingi 700,000/- kwa wiki kwa huduma ya choo ni kidogo ukilinganisha na idadi ya watu wanaotumia stendi ya Tabora.

Aliwataka watendaji kujifunza kutoka Halmashauri ya Mji Nzega ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato katika huduma ya choo katika stendi yao.

Post a Comment

0 Comments