TAARIFA KWA UMMA
Kama mnavyofahamu Serikali
inaendelea na Mchakato wa kuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii baada
ya Sheria kupita Bungeni.
Hivi karibuni kumeibuka taarifa ambazo si
sahihi kuhusiana na usalama wa michango na mafao ya Wanachama.
Taarifa
hizi zimepelekea baadhi ya Wanachama na Wastaafu kuwa na wasiwasi kuhusu
hatma ya michango na mafao yao.
Mamlaka inapenda kuwaondoa
wasiwasi Wanachama na Wastaafu wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuwa
mafao na michango yao iko salama.
Waajiri wanapaswa kuendelea kupeleka
michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii husika.
Vile
vile Wanachama na Wastaafu waendelee kufuatilia mafao yao katika Mifuko
kama kawaida hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Dar es Salaam
Tovuti: www.ssra.go.tz
05/03/2018
0 Comments