Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
anayeshughulikia watoto na Migogoro ya Kivita Virginia Gamba akizungumza
na Meja Afred Mwinuka wakati alipotembelea kambi ya Wanajeshi kutoka
jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani
chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID
Shangilitobaya Jimboni Darfur Nchini Sudan.
Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
anayeshughulikia watoto na Migogoro ya Kivita Virginia Gamba akizungumza
na Meja Afred Mwinuka wakati alipotembelea kambi ya Wanajeshi kutoka
jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani
chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID
Shangilitobaya Jimboni Darfur Nchini Sudan .
Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na
Umoja wa Afrika UNAMID wakiwa katika Doria maeneo ya Jirani na Mlima
Mawe Khor Abeche Jimboni Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni
Selemani Semunyu).
Na Luteni Selemani Semunyu UNAMID
Umoja wa mataifa UN umeipongeza
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Magufuli
na Mkuu wake wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kufuatia
jitihada zao za kudumisha amani ndani na Nje ya Nchi hiyo.
Hayo yalibainishwa na mwakilishi
Malum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya
Watoto (Special Representative of Secretary general of Child Abuse and
AA) Profesa Virginia Gamba wakati wa Ziara yake kikazi katika Maeneo ya
vjiji vya Shangilitobaya Jimboni Darfur nchini Sudan hivi Karibuni.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa
nchi ya kuigwa Afrika zinazopiga hatua kubwa ya maendeleo zinazopaswa
kutiliwa mfano lakini yote hiyo inatokana na umadhubuti wa Serikali
yake, na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa mchango wake
katika kushughulikia mambo ya msingi katika kudumisha Amani.
“Sina budi kuipongeza Serikali
chini ya rais John Magufuli inafanya kazi nzuri na Mkuu wa majeshi ya
Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kwani utendaji wao ni wa kutukuka Afrika
nzima katika kuleta Amani kwani bila Amani hakuna maendeleo hivyo
maendeleo yanayotarjiwa Tanzania ytapatikana kwa sababu ya Amani”
Alisema Profesa Virginia.
Aliongeza kuwa kutokana na
kuimarika kwa Amani ni rahisi kwa nchi yeyote kujiletea maendeleo haraka
na kuwataka kuendeleza jitihada hizo kwa kuwalinda watoto ambao ni nusu
ya Idadi ya watu Duniani hivyo wakilindwa Watoto Dunia itakuwa salama.
“ Najivunia Tanzania naweza
kujiita mi ni rafiki wa Tanzania sio kwa sababu nyingine ni kutokana na
Umahiri wao katika Amani ikiwemo jeshi lake la Ulinzi limekuwa Msaada
mkubwa katika kuleta Amani kupitia Umoja wa Mataifa” Alisema Profesa
Virginia.
Pia aliwataka Wananchi wa Sudan
kuiga Mfano wa Tanzania waliowasha mwenge katika kilele cha Mlima
Kilimanjaro kuwa ishara ya Amani Afrika na kumulika dhidi ya maovu mbali
mbali ikiwemo dhidi ya watoto kwa kuwasha moto wa amani utakaoangazia
watoto wote wa Sudan.
Aliongeza kuwa ni wajibu wa
Sudan kuuiga Tanzania kwa kuwasha moto wa Amani kwani wana kila sababu
ya kufanya hivyo bila kutegemea msaada wowote kwani ni nchi yenye
rasilimali nyingi za kiuchumi lakini kinachokwamisha ni Amani ili
kujiletea maendeleo.
Mwakilishi huyo wa Umoja wa
mataifa mbali na kutembelea vijiji mbalimbali alitembelea kambi ya
Shangilitobaya inayokaliwa na Kikosi cha Tanzania chini ya kikosi cha 11
kinachoongozwa na Kanali William Sandy na kuwapongeza Askari wake kwa
kazi nzuri ya Ulinzi wa Amani Duniani kote.
Tanzania kupitia Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania linashiriki katika mpango wa Ulinzi wa Amani
chini ya Mwamvuli wa Umoja wa mataifa na Umoja wa Afika UNAMID nchini
SUDAN ambayo sasa inaingia hatua ya Pili ambayo majeshi ya Tanzania
yameunganihswa katika kikosi maalum ambacho kinaanza kazi katika safu za
Milima ya jebel Marra Mashariki maeneo ambayo hayakunufaika kwa
kufikiwa na UNAMID kwa kipindi chote.
Wanajeshi wa Tanzania hivi
karibuni walipongezwa kuyafikia maeneo ya safu za Milima ya Jaber Mara
na kufanya Doria ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa UNAMID na mashirika
ya Umoja wa Mataifa kutokana na maeneo hayo kukaliwa na Waaasi na ubovu
wa Miundombinu.



0 Comments